Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: HAFLA YA TANZANIA BLOGGERS NETWORK ILIVYOFANA SERENA HOTEL JIJINI DAR

Sehemu ya Wamiliki wa Blogs mbali mbali hapa nchini wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni Rasmi katika hafla maalum ya mwaka kwa Tanzania Bloggers Network,ambaye ni Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT),Ndg. Kajubi Mukajanga pamoja na baadhi ya wadhamini waliofanikisha hafla hiyo,iliyofanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam.

Mgeni Rasmi katika hafla maalum ya mwaka kwa Tanzania Bloggers Network,Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT),Ndg. Kajubi Mukajanga (wa pili kulia) akizungumza jambo na baadhi ya Wamiliki wa Blogs Tanzania,waliokutana pamoja leo kwa lengo la kufahamina na kuunganisha vyema umoja wao.

Mkurugenzi wa Masoko kwa Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu,Kelvin Twissa akizungumza machache katika hafla hiyo.

 Mkongwe kwa maswala ya kublog hapa nchini,Ankal Issa Michuzi akifafanua jambo kwa wageni waalikwa toka Ubalozi wa Marekani juu ya kukutana kwao kwenye hafla hilo iliyofanyika usiku huu kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar es salaam.

Picha ya pamoja kwa baadhi ya Wanablog na wadhamini wa hafla hiyo.

Nadeem wa Aim Group (kulia) akiwa na maafisa kutoka ubalozi wa Marekani waliohudhuria


Suri na Kamera imo??

Ras Jhikoman akiimba wimbo wake mpya unaolaani mauaji ya Albino. Mwanamuziki mkongwe na blogger na MC wa siku hii Anko John Kitime anamshikia mike

Ras Jhikoman akilia na wauwaji wa Albino

Ankal akishusha mistari kwa wageni

Mgeni rasmi akisalimiana na Shafiq Mpanja wa Aim Group

Mike Mushi wa Jamii Forum (shati la draft) akiwa na Krantz Mwantepele (kulia) Shafiq Mpanja wa Aim Group (shoto) na mdau

Meza ya Jay Millions ya VODACOM

Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa akiwa na vingunge wa Aim Group
Mgeni Rasmi Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania Mhe Kajubi Mukajanga (kati) akiwa na Ankal na Anko John Kitime

Kutoka kushoto ni Woinde Shizza, Othman Michuzi, Pam Mollel, Zainul Mzige  na Karim

Mgeni Rasmi Mhe Kajubi Mukajanga akikata ndafu wa TBN. Kushoto kwake ni mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani na kulia ni Kelvin Twissa, Mdhamini mkuu wa Mnuso huo pamoja  na Rachel Pallangyo wa TBN

Mkuu wa ukumbi (floor manager) Monica Joseph Mara akiongoza wana TBN kuserebuka


Ankal akiwa na ubavu wake (kulia) na ubavu wa Bongo Celebrity a.k.a Mama Amaya

Nyota wa mchezo hapa ni Gadiola toka Arusha (mbele kati)

Msoma risala mkuu wa TBN Henry Mdimu akiwa na bloggers wenzie

Wana TBN katika picha ya pamoja

Ankal akiwa na Max wa Jamii Forums ambao wote ni waasisi wakuu wa TBN


Nyota hapa ni blogger toka Bukoba Ruta (Blue T-shirt) akiwa na blogger wa Dar, Arusha  na Kilimanjaro

Mwanachama mkongwe wa TBN Kaka Omar Swai (wa pili kushoto) akiwa na wana libeneke toka Arusha Pam Mollel (shoto), Woinde Shizza (kulia) na Mama Ankal

MAPICHA ZAIDI
LINK 1
LINK 2

LINK 3

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO