Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MFANYABIASHARA MMOJA MAARUFU JIJINI ARUSHA AOKOTWA AKIWA MTARONI AKIWA AMEFARIKI

 

LiberatusSabas_1

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas (pichani), amemtaja mfanya biashara huyo kuwa ni Obed Masawe, (50) ambae anamiliki duka la kuuza vinywaji vikali ,maarufu Masobe Treders, lililopo jengo la Chama cha Mapinduzi CCM, Mkoa wa Arusha.

Amesema mfanyabiashara huyo ambae ni mkazi wa Njiro jijini Arusha,alifikwa na mauti akiwa kwenye klabu ya wafanyakazi wa Benki kuu ya Tanzania, BOT,alipokuwa akiendelea kunywa bia.

Sabasi amesema tukio hilo limetokea Machi 23 mwaka huu, majira ya saa 1.30 usiku,ghafla alijisikia vibaya, na taarifa za awali zinaonyesha kuwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa presha.

Katika tukio lingine Kamanda, Sabas, amesema mwanamke mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 25, alikutwa amefariki dunia na mwili wake kusokomezwa kwenye mtaro wa maji ya mvua jana, katika makutano ya bara bara ya Makongoro na Azimio, jirani na jengo

la CCM Mkoa.

Amesema mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa hospital ya mkoa ya Mount Meru, ukisubiri ndugu kujitokeza kumtambua.

Ameongeza kuwa marehemu huyo ambae hajafahamika, mwili wake uligundulika baada ya kutoa harufu .

Uchunguzi unaendelea kufahamu vyanzo vya vifo hivyo.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO