Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

JAMES MBATIA AZINDUA KAMPENI KWA KISHINDO, MSAFARA WAKE WAISIMAISHA VUNJO

Msafara wa Pikipiki ukimsindikiza mgombea Ubunge katika jimbo la Vunjo kupitia chama cha NCCR-Mageuzi na UKAWA ,James Mbatia wakati wa kwenda kufanya uzinduzi wa Kampeni katika jimbo jilo.
Msululu wa magari ukimsindikiza mgombea huyo.
Maeneo mbalimbali aliyopita mgombea huyo alipokelewa na makundi mbalimbali ya watu waliokuwa wamesimama kando ya barabara wengi wao wakiwa ni kina mama.


Katika maeneo mengine wananchi walisimamisha msafara wake na kusalimia kwa muda kabla ya kuendelea na safari.
Shughuli zilisimama kwa muda katika maeneo mbalimbali angalau kutoa nafasi japo kupunga mkono kwa mgombea huyo.
Msafara ukielekea uwanja wa Michezo wa Chuo cha Ualimu cha Marangu kwa ajili ya uzinduzi wa mkutano wa Kampeni.
Makondakta na madereva wa daladala katika eneo la Marangu mtoni wakisalimiana na mgombea ubunge katika jimbo la Vunjo ,James Mbatia.
Hii ndivyo ilivyokuwakatika eneo la Marangu Mtoni.
Raia wa kigeni wakichukua taswira za mgombea Ubunge katika jimbo la Vunjo,Jmaes Mbatia.
Mgombea Ubunge katika jimbo la Vunjo James mbatia kaiwa ameongozana na mkewe ,Catherine Mbatia na motto wao Chelsea wakiingia katika uwanja wa michezo wa chuo cha Ualimu Mrangu kwa ajili ya mkutano wa ufunguzi rasmi wa kampeni.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini (0755 659929)
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO