Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

HATARI: BEKI MANCHESTER UNITED LUKE SHAW AVUNJIKA MGUU UWANJANI TIMU YAKE IKICHAPWA NA PSV YA UHOLANZI

KOCHA wa Manchester United, Louis van Gaal amesema kwamba beki wake Luke Shaw atakuwa nje mwa muda usiopungua miezi sita baada ya kuumia jana katiia mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya wenyeji PSV nchini Uholanzi.

Katika mchezo huo ambao United ililala 2-1, Shaw alimwaga machozi wakati wanatolewa nje kutokana na uchungu wa maumivu makali kutokana na kuvunjika mguu wake wa kulia.

Dunia ya soka iliungana usiku wa jana baada ya beki wa PSV Eindhoven, Hector Moreno kumvunja mara mbili mchezaji wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 20 mguu wa kulia.

Shaw aliwekewa hewa ya ziada na kupatiwa huduma ya kwanza uwanjani mjini Eindhoven kabla ya kukimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi. Atarejeshwa Manchester leo na Alhamisi anatarajiwa kufanyiwa upasuaji.

Manchester ‘who’? United, lakini sio imara! Maana imepiteza ugenini dhidi ya PSV ya Uholanzi.Pamoja na kutangulia kupata bao kupitia Memphis Depay, imejikuta ikilala kwa mabao 2-1.

Depay ndiye alianza kuiadhibu timu yake ya zamani kabla ya wenyeji hao kuchangamka na kutupia bao mbili.

Man United walionekana kuchamka katika kpindi cha kwanza lakini mambo yakawa hovyo kipindi cha pili.

Kukosekana kwa Wayne Rooney ambaye ni mgonjwa kulionekana ni tatizo hasa katika safu ya ushambuliaji.

PICHA NA VYANZO VYA KIMATAIFA

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO