Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mgombea Mwenza CCM Avunja Ngome ya ACT Tanga, Avuna Wanachama 272 wa Upinzani

Baadhi ya wana CCM na wananchi wakiwa wamefurika katika Viwanja wa Jitegemee Mjini Muheza ambapo mgombea mwenza nafasi ya urais CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alifanya mkutano wa kampeni leo.
Baadhi ya wana CCM na wananchi wakiwa wamefurika katika Viwanja wa Jitegemee Mjini Muheza ambapo mgombea mwenza nafasi ya urais CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alifanya mkutano wa kampeni leo.
Mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya Usagara Tanga Mjini leo. Idadi kubwa ya wananchi walihudhuria mkutano huo hadi wengine kuzimia kutokana na msongamano.
 
Baadhi ya wana CCM na wananchi wakiwa wamefurika katika Viwanja wa Jitegemee Mjini Muheza ambapo mgombea mwenza nafasi ya urais CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alifanya mkutano wa kampeni leo.
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM Kitaifa, Bi. Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi kwenye moja ya mikutano ya kampeni za CCM timu ya mgombea mweza iliyofanyika mkoani Tanga leo.
Baadhi ya vijana wakiwa wamepanda juu ya gari ili kumsikiliza mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan katika Jimbo la Mkinga.
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimamishwa na wananchi njiani alipokuwa akielekea katika Jimbo la Mkinga kufanya mkutano wa kampeni.
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimamishwa na wananchi njiani alipokuwa akielekea katika Jimbo la Mkinga kufanya mkutano wa kampeni.
Sehemu ya wanaCCM na wananchi ikiwa imemsimamisha barabarani mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kumsikiliza alipokuwa njiani kuelekea kwenye mikutano mikubwa ya kampeni.
 
MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan amevunja ngome ya chama cha ACT Wazalendo Mkoani Tanga pamoja na kuvuna wanachama 272 kutoka vyama mbalimbali vya upinzani baada ya wanachama wa vyama hivyo kujiunga rasmi na CCM.
 
Bi. Samia Suluhu ambaye ni mgombea mwenza wa Dk. John Pombe Magufuli amefanikiwa kuvunja ngome za wapinzani leo mjini Tanga katika mikutano yake ya kampeni baada ya wagombea udiwani watano wa ACT Wazalendo kujiunga na CCM pamoja na wanachama wengine 235 toka Tanga mjini kujiunga na CCM kwenye mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Usagara mkoani Tanga.
 
Akihutubia katika mkutano mkubwa wa kampeni kunadi ilani ya CCM Tanga mjini uwanja wa Usagara, Bi. Samia Suluhu aliwapokea wagombea udiwani watano kutoka ACT Wazalendo, wakiwemo Wilson Elia (wa Kata ya Duga), Gasper Maboko (Kata ya Nguvumali), Charles Luanda (Maweni) na Marry Scoty (Kata ya Tanga Sisi) pamoja na Sada Mbwambo (viti maalum).
 
Mbali na madiwani hao kukihama chama cha ACT, wanachama 235 kutoka ACT, CUF na Chadema walijiunga na CCM kwenye mkutano huo wa Tanga mjini huku wengine 37 wakijiunga na CCM katika mkutano mwingine ulofanyika Jimbo la Muheza hivyo kutimiza wanachama 272 wapya kujiunga katika mikutano ya siku hiyo.
 
Akizungumza na wanaCCM na wananchi waliojitokeza mkutano wa Tanga Mjini, Bi. Suluhu aliwaomba kuichagua CCM kurudi madarakani ili kuendeleza maendeleo iliyofikia katika maeneo mbalimbali, ikiwemo huduma za kijamii na miundombinu hasa ya barabara. Alisema wapinzani hawafai kupewa madaraka kwa kuwa hawajajipanga kimfumo kwani hata viongozi wanaogombea wamekimbia vyama vyao na wanachotaka ni maslahi yao zaidi.
 
Alisema kwa mkoa wa Tanga Serikali ya CCM imepanga kuyakagua mashamba makubwa yaliotwaliwa na wawekezaji na kutelekezwa kisha kuyarejesha kwa wananchi ili waweze kuyatumia kwa uzalishaji, ikiwa ni pamoja na kupanua bandari ya mkoa huo kuchochea maendeleo.
 
Aidha aliongeza kuwa wakulima wa zao la korosho hawana budi kuongeza uzalishaji na kutokata tamaa kwani tayari Serikali inafanya mazungumzo na Serikali ya Norway kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho mkoani hapo ili kuongeza thamani ya zao hilo. Alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha asilimia 40 ya vijana wanapata ajira kwenye viwanda vitakavyo jengwa maeneo anuai ya nchi.
 
Bi. Samia alifanya mikutano minne mikubwa katika majimbo ya Mkinga, Pangani, Mheza na Tanga Mjini na mikutano midogo midongo sita alioifanya njiani akisimamishwa na wananchi wakitaka kumsikia alipokuwa akipita. Hata hivyo katika mkutano wake wa Tanga Mjini baadhi ya wananchi walizidiwa kutokana na msongamano na idadi kubwa ya watu na kuzimia kabla ya kupewa huduma ya kwanza.

Gari ya Bi. Samia Suluhu ikitoka kwenye kivuko cha Mv. Pangani II mara baada ya kuvushwa, mgombea huyo mwenza wa urais CCM alikuwa akitoka kwenye mkutano wa hadhara JImbo la Pambani leo.
Kutoka kushoto ni mgombea ubunge Jimbo la Pangani, Jumaa Hamid Aweso, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Pangani, Hamis Mnegero na Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan wakizungumza jambo.
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akizungumza na wanaCCM na wananchi kwenye mikutano ya hadhara leo katika baadhi ya Majimbo ya Mkoa wa Tanga.
Moja ya ahadi za CCM msimu wa Rais Jakaya Kikwete ikiendelea na ujenzi wa gati Wilayani Pangani ikiendelea na ujenzi
Bi. Samia Suluhu akishuka ndani ya kivuko mara baada ya mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Mwera Jimbo la Pangani.
Bi. Samia Suluhu akihutubia mkutano wa kampeni Muheza.

Baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na CCM wakiwa katika msitari mara baada ya kurejesha fomu.
Sehemu ya wanaCCM na wananchi ikiwa imemsimamisha barabarani mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kumsikiliza alipokuwa njiani kuelekea kwenye mikutano mikubwa ya kampeni.

Sehemu ya wanaCCM na wananchi ikiwa imemsimamisha barabarani mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kumsikiliza alipokuwa njiani kuelekea kwenye mikutano mikubwa ya kampeni.
Bi. Samia Suluhu akiwa na mgombea ubunge wa Jimbo la Tanga Mjini Omary Nundu(kulia).

Mmoja wa wananchi wakipewa huduma ya kwanza mara baada ya kuzimia kutokana na msongamano katika mkutano wa kampeni kwa  mbaya.
Mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza Tanga Mjini leo.

Mgombea Ubunge wa CCM, Jimbo la Bumbuli, January Makamba akizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni.
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akizungumza na wanaCCM na wananchi kwenye mikutano ya hadhara leo katika baadhi ya Majimbo ya Mkoa wa Tanga.

Mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza Tanga Mjini leo.

*Imeandaliwa/www.thehabari.com
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO