Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

LOWASSA AZINDUKA KAMPENZI ZA UBUNGE WA MBOWE JIMBONI HAI.. ONA TASWIRA HALISI HAPA

 

Mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi nchini UKAWA Edward Lowasa, ameahidi kuhakikisha anapambana na tatizo la rushwa ambalo limekuwa chanzo cha umasikini nchini.
Siku 29 pekee kuelekea oktoba 25 mwaka huu, sauti bado ni ile ile kila kona ya nchi akiwa mjini hai ambapo alihutubia mikutano ya hadhara katika maeneo ya lunongai, shirimatunda, machame na hai mjini Edward Lowasa amesema atahakikisha anaongoza nchi kwa misingi ya haki na usawa huku akiahidi kutumia vema ilani ya ukawa kuhakikisha anapambana na rushwa kwani kwa muda mrefu imekuwa kikwazo kwa maendeleo ya nchi huku wachache wakinufaika na rasilimali za nchi.
Huku akionekana kujiamini kushinda katika uchaguzi ujao, Freeman Mbowe anayewania nafasi ya ubunge katika jimbo hilo la hai amewataka wanahai na watanzania kwa ujumla kuhakikisha wanafanya mabadiliko kwani ndio njia pekee ya kujikwamua na umasikini uliokithiri hasa kwa wananchi wa kipato cha chini.
Fredrick Sumaye waziri mkuu mstaafu akihutubia maelfu wakazi wa jimbo la hai amesema ni wakati muafaka wa kukiondosha chama cha CCM madarakani kwani kimeshindwa kusimamia rasilimali za nchi na kufanya nchi kuendelea kuwa masikini.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokelewa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, wakati alipowasili eneo la Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mpira wa Machame, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mpira wa Machame, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.

Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, Mh. James Mbatia akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015.

Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015.

Picha kwa hisani ya Othman Michuzi

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO