Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Udiwani Sombetini Arusha: Bananga azidi “Kuchanja Mbuga”, Afanya Mkutano Mtaa wa hasimu wake na kuvuna viongozi na wanachama wa Tawi zima la CCM Sombetini

SAM_6429

Wananchi wa Mtaa wa Majengo Chini, Kata ya Sombetini wakimsikiliza kiongozi wa Tawi la CCM Sombetini akikabidhi bango la tawi lao kwa Katiu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, Mh Kalist Lazaro katika mkutano wa kampeni kumnadi mgombea udiwani Kata ya Sombetini kupitia CHADEMA Mh Ally Bananga.

SAM_6410
Mgombea Udiwani Sombetini akijinadi kwa wananchi kuomba kuchaguliwa tena baada ya kuwaongoza kwa mwaka mmoja na nusu katika Kata ya Sombetini Jijini Arusha. Mkutano huo ulifanyika jana jioni katika Mtaa wa Majengo Chini, eneo ambalo liko chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Mtaa atokanaye na CHADEMA Godfrey Kitomari aliye kwenye msuguano mkali na Bananga baada ya kuzidiwa katika uteuzi wa mgombea udiwani ndani ya chama hicho.

Kitomari analalamikizwa kufanya kampeni hasi dhidi ya mwanachama mwenzake katika Kata hivyo, lakini akihutubia mkutano huo Katibu wa CHADEMA Mkoa alieleza wanachama wa chama chake kutopoteza muda na waliosaliti au ambao wana dhamira zakusaliti kwasababu mabadiliko hayasubiri mtu yeyote. Alienda mbali zaidi na kutolea mfano wa viongozi wakubwa wa UKAWA kama Prof Lipumba na Dr SLaa walivyosaliti lakini umma uliwapuuza ndani ya muda mfupi.

SAM_6376

Kiongozi mwakilishi wa CHADEMA idara ya intelijensia Taifa alipata wasaa wa kusalimia wananchi wa Sombetini mkutanoni hapo na kuwaombea kura wagombea wote wa Udiwani (Bananga) Ubunge (Godbless Lema) na Urasi (Lowassa)
Alitumia nafasi hiyo pia kuwatoa hofu wananchi kuwa uchaguzi utakuwa wa amani na hakutakuwa na vurugu ya aina yeyote na kwamba wameshakubalina na Tume ya Uchaguzi, Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama kuwa matokeo yote ya kuanzia udiwani, ubunge na urais yatabandikwa kwenye mbao za matokeo mara baada ya kuhesabiwa ili kuepusha nchi na hatari ya kuvurugika amani.

SAM_6397

Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, Mh Kalisti Lazaro akihutubia mkutanoni hapo ambapo alimpiga vijembe mshindani wa Godbless Lema, ambaye ni mgombea Ubunge wa Arusha Mjini kupitia CCM Philemon Mollel almaarufu Monaban kuwa anawadanganya wanawake kuwapa mikopo wakati yeye mwenyewe anadaiwa na bank zaidi ya bilioni 3.

Lazaro “Bush” ni mgombea Udiwani kata ya Sokoni I lakini alidai hana mtu wa kushindana naye ndio maana anashiriki kamapeni maeneo mengine.

SAM_6401

Baadhi ya wagombea udiwani wa CHADEMA kwa Jimbo la Arusha Mjini wakisalimia wananchi kwa pamoja baada ya kutambulishwa katika mkutano huo

SAM_6409

Ally Bananga akisimulia baadhi ya amambo aliyotekeleza kwa kipindi cham mwaka mmoja na nusu aliokuwa Diwani wa Sombetini na kueleza mafanikio yake kwa utatuaji kero ya madawati kwa shule za msingi, uboreshaji miundo mbinu na ujenzi wa madarasa kwa ajili ya watoto kupata pa kusomea. Katika Mtaa wa Majengo alisimulia namna kero ya mtaro wa maji inavyosumbua na kuahidi kuendelea pale alipoishia kutafuta ufumbuzi kamili kwa kuwashirikisha TANROADS ambao walidaiwa kuwa wahusika wakuu wa mtaro huo.

SAM_6427

Kiongozi wa Tawi la CCM Sombetini akitoa maelezo kwa wnanchi na kueleza kuwa wamehamia CHADEMA tawi zima ili kukimbizana na kiu ya Mbadiliko waliyonayo watanzania wengi nchini. Baadae alikabidhi bango lao na kuruhusu wanachama kulitumia wapendavyo. Baadhi walianza kuligombania na kutaka kulichoma moto hapo hapo lakini viongozi wa CHADEMA waliwazuia.

SAM_6435

Wananchi wakigombana kulichanchana bango la wanaCCM waliohamia CHADEMA jana

SAM_6437

tabasamu la furaha baada ya kuhamia CHADEMA

SAM_6440

Mgombea Udiwani Sombetini Ally Bananga na Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Kalist Lazaro wakiondoka eneo la mkutano baada ya kuahirishwa na kusindikizwa na umati wa watu

SAM_6441

Timu ya mgombea Udiwani Bananga ikiondoka eneo la mkutano

SAM_6442

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO