Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

SIMANZI: MGOMBEA UBUNGE CHADEMA JIMBO LA LUSHOTO BWA MOHAMED MTOI AFARIKI DUNIA KWA AJALI

Huku kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, 2015, Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimepata pigo baada ya mgombea wake Jimbo la Lushoto Mkoani Tanga, ambaye pia alikuwa Mratibu wa Kanda ya Kaskazini kwa chama hicho, Bw Mohamed Mtoi kufariki dunia kwa ajali ya gari.

Kwa mujibu wa sheria za uchaguzi, inapotokea mgombea amefariki Msimamizi wa Uchaguzi huitaafiru tume ya Uchaguzi kwa ajili ya kupanga tarehe nyingine ya uchaguzi na chama kilichopoteza mgombea kupendekeza mgombea mwingine.

Blogu hii inatoa pole kwa wafiwa wote na Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peopni.

IFUATAYO NI TAARIFA YA RAMBIRAMBI TOKA CHADEMA BLOG SAMBAMBA NA MATUKIO YA MAREHEMU ENZI ZA UHAI WAKE.

“Nachukua fursa hii kwa masikitiko makubwa sana kutoa Salamu za Rambirambi kwa Familia na Uongozi wa Juu wa Chadema Makao makuu kwa msiba wa Kamanda mwenzetu, Mpiganaji wa kweli, Kijana mwenzetu Ndugu Mohamed Mtoi Kanyawana aliyefariki kwa ajali ya Gari iliyotokea huko Tanga. Kwa kweli bado tulikuwa tunamhitaji sana kamanda mwenzetu lakini kifo ni mpango wa Mungu ametangulia mbele sisi tupo nyuma yake. Tunajua mchango wake wa kujenga Chama na tunauthamini sana. Mohamed Mtoi alikuwa ni tegemeo letu kwenye nafasi ya Ubunge Jimbo la Lushoto pia kama mratibu wa Kanda ya Kaskazini, hivyo tumepata pigo kubwa sana hasa katika kipindi hiki kigumu kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu. Tulikuwa tunashirikiana sana na Ndugu Mohamed Mtoi kwenye kusambaza Taarifa Mbalimbali za Chama, mchango wake ulikuwa mkubwa sana. Mungu aiweke roho ya Marehemu Mohamed Mtoi Kanyawana mahali Pema Peponi.
Wenu ChademaBlog Admin”


Picha ya kampeni ya Mohamed Mtoi wakati anagombea Jimbo la Lushoto Tanga

Pichani Gari ambayo ndugu Mohamed Mtoi Kanyawana amepatia ajali akitokea kwenye kampeni

Mohamed Mtoi akiwa na familia yake


Mohamed Mtoi akiwa shule ya msingi 1993

Mohamed Mtoi akiwa kiranja shule ya msingi 1990

Kamanda Mohamed Mtoi akiwa na makamanda wenzake kwenye mkutano mkuu wa Chadema


Kamanda Mohamed Mtoi akiongozana na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mheshimiwa Freeman Mbowe kwenye harakati za kujenga Chama.

Kwa kweli tumempoteza kamanda wa Ukweli kabisa aliyekuwa na mapenzi mema na chama. Mungu akupumzishe mahali pema peponi


Kamanda Mohamed Mtoi akiwa na mtoto wake

Kamanda Moohamedi Mtoi akiwa ziarani barani Ulaya

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO