Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAGUFULI AMALIZANA NA KAMPENI ZAKE KAGERA,KESHO KUUNGURUMA MKOANI GEITA.


 Wananchi wa mji wa Ngara na vitongoji vyake wakiwa wamefurika kwenye viwanja vya posta mjini humo,huku wakishangilia wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao na kuwaomba ridhaa ya kuwa Rais na kuiongoza nchi Tanzania katika awamu ya tano.Dkt Magufuli amekamilisha mikutano yake ya kampeni zake katika mkoa wa Kagera wenye jumla ya majimbo 9 ya Uchaguzi. PICHA NA MICHUZI JR-KAGERA
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Posta,wilayani Ngara jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.Dkt Maguful kwa siku mbili mfululizo ameweza kukamilisha mikutano yake kwenye Wilaya  zote za Mkoa wa Kagera,ambapo kesho anaelekea mkoani Geita kwa ajili ya kujinadi kwa wananchi wa mkoa huo ili waweze kumpigia ya kuwa Rais wa awamu ya tano,katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwafafanulia kwa umakini mkubwa alipokuwa akiwahutubia wananchi katika uwanja wa shule ya sekondari Rumanyika,wilayani Kyerwa mapema leo mchana mkoani Kagera kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Sehemu ya umati wa watu ulikuwa umefika kwenye mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli uliofanyika mapema leo mchana kwenye uwanja wa shule ya sekondari Rumanyika,wilayani Kyera mkoani Kagera.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika uwanja wa shule ya sekondari Rumanyika,wilayani Kyerwa mapema leo mchana mkoani Kagera kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Wakazi wa Ngara na vitongoji vyale waliokusanyika kwenye viwanja vya Posta mjini Ngara jioni ya leo wakishangilia jambo,wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Posta,wilayani Ngara jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Wananchi wa Ngara wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa kampeni
  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akisisitiza jambo alipokuwa akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Posta,wilayani Ngara jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Kayanga,Karagwe mjini asubuhi hii kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Mashujaa mjini Misenyi asubuhi hi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
 wakazi wa mji wa Misenyi  katika viwanja vya mashujaa wakishangilia huku wakiendelea kumsikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,alipokuwa akijinadi kwa kumwaga sera zake na kuomba watanzania wamchague kwa ridhaa yao ili awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu ya Tano
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO

Don't Forget To Like Our FacebookPage
×
Click Here To Visit our Page