Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Maalim Seif na CUF Wazindua Rasmi kampeni za Urais Zanzibar Jana

Maalim Seif akiongoza ufunguzi wa Kampeni hizo.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na Mgombea Urais wa Ukawa wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati wa Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za CUF, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Demokrasia, Kibanda Maiti, Zanzibar leo Septemba 9, 2015.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akizungumza jambo na Mgombea Mwenza wake, Mh. Juma Duni Haji, katika hafla ya Ufunguzi wa Kampeni za Chama cha Wananchi CUF - Zanzibar, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Demokrasia, Kibanda Maiti, Zanzibar leo Septemba 9, 2015.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF - Zanzibar, Nassor Mazrui, wakati akiwasili katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Demokrasia, Kibanda Maiti, Zanzibar leo Septemba 9, 2015

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akilakiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA-Zanzibar, Salum Mwalim, wakati akiwasili katika Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za Chama cha Wananchi CUF - Zanzibar, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Demokrasia, Kibanda Maiti, Zanzibar leo Septemba 9, 2015.

Mgombea Mwenza wa Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Juma Duni Haji, akiwasalimia wazanzibar.

Picha kwa Hisani ya Othman Michuzi

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO