Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

RAIS KIKWETE ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WAPYA MONDULI JANA

 


Amiri Jeshi Mkuu Dkt.Jakaya Mrisho akiwa katika gari maalum la wazi na Mkuu wa Chuo cha maafisa wa Jeshi(TMA) Monduli akiingia katika uwanja wa paredi tayari kwa kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi jana.


Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Adolf Mwamunyange akimkaribisha Amiri Jeshi mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika chuo cha jeshi Monduli(TMA) ili kutukunu kamisheni kwa maafisa wapya jana.


Maafisa wapya wa Jeshi wakila kiapo mbele ya Amiri jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.


Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Adolf Mwamunyange akimkaribisha Amiri Jeshi mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika chuo cha jeshi Monduli(TMA) ili kutukunu kamisheni kwa maafisa wapya jana.


Amiri Jeshi Mkuu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi katika Chuo cha Jeshi(TMA) Monduli Mkoani Arusha jana.


Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akimkabidhi Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete zawadi ya picha akiwa katika gari la wazi katika sherehe za awali chuoni hapo, na kitara pamoja na nembo maalum ya jeshi kwa kutambua mchango wake katika kuliboresha na kulifanya la kisasa Jeshi la Wananachi wa Tanzania wakati wa Sherehe za kutunuku l\kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi katika chuo cha jeshi Monduli jana.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiiangalia picha ya kuchora ya Mkewe Mama Salma Kikwete aliyoipokea kwa niaba yake


Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride muda mfupi kabla ya kutunuku Kamisheni kwa maafisa wapya wa Jeshi katika Chuo cha Jeshi Monduli.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi Afisa mwanafunzi bora Luteni Usu Antony Shija wakati wa sherehe za kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya leo katika chuo cha jeshi TMA Monduli.


Amiri Jeshi Mkuu Rasi Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa akimpa zawadi afisa mwanafunzi bora wa kike Luteni Usu Martina James Shija wakati wa sherehe za kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi katika chuo cha jeshi Monduli jana. PICHA NA IKULU

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO