Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

NAWASHANGAA MAWAZIRI WAKUU WENZANGU WALIOSTAAFU,WAKIDAI CCM MIAKA 50 HAKUNA KILICHOFANYA-JAJI WARIOBA

 Waziri Mkuu Mstafu Jaji Joseph Sinde Warioba akihutubia wakazi wa Butiama ambapo aliwaeleza Magufuli anafaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MARA

WAZIRI Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, ameibuka katika kampeni za mgombea urais wa CCM Dk. John Magufuli na kusema kuwa anashangazwa na hatua ya mawaziri wakuu wenzake kuhama CCM na kudai hakuna kilichofanyika katika miaka 54 ya Uhuru.

Pamoja na hali hiyo amesema anajua wazi huenda hata wanachokifanya hawajui wajibu wao walipokuwa katika madaraka hayo kama washauri wakuu wa rais.alisema  sasa umefika wakati wa watu wanaomtumia kama dira Baba wa Taifa katika kampeni zao wajitafakari zaidi.

"Wengine katika kampeni zao wanatumia maneno ya Mwalimu kama wamechanganyikiwa. Huwezi kumtumia Mwalimu kama dira halafu unasema CCM haijafanya kitu, aliijenga Tanzania kwenye misingi na wote walimfuata wanapita kwenye misingi yake," alisema Jaji Warioba
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika mjini Bunda leo.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akipokea kifimbo na Chief Japhet Wanzagi kwa niaba ya Wazee wa Butiama.
 Dkt akionesha fimbo hiyo aliyokabidhiwa na Chief wa Wazanaki,Japhet Wanzagi
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea ubunge kulia ni Nimrod Mkono kutoka jimbo la Butiama Vijijini na  Profesa Sospeter Muhongo ambaye anatoka jimbo la Musoma vijijini.

 Mamia ya Wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli.
 Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Nyamuswa ambako ndiko alikozaliwa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba,wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mgombea Ubunge wa jimbo la Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe. Stephen Wasira,shoto ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba,kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika mjini Nyamuswa jioni ya leo.
 Wananchi wa Nyamuswa wakimsikiliza Dkt Magufuli.
 Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Nyamuswa ambako ndiko alikozaliwa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba,wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake na kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisalimiana na mgombea ubunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Ndugu Sospeter Muhongo,kushoto ni Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe. Stephen Wasira wakati wa mapokezi mkoani Mara,pichani kati ni Mtoto wa Baba wa Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Afrika Mashariki,Mh Makongoro Nyerere
  Umati wa wakazi wa Butiama wakimsikiliza Mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Sehemu ya Wananchi wa Butiama wakishangilia jambo

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO