Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WAZIRI MKUU PINDA AKABIDHI MAGARI YA KUBEBEA WAGONJWA JIJINI ARUSHA LEO YENYE THAMANI YA MIL 150

Waziri  mkuu wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mizengo Pinda akiwa anakata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua magari ya kubeba  wagonjwa ambayo ameyakabidhi leo  mkoani Arusha kwa ajili ya kupelekwa wilayani Ngorongoro kwa ajili ya kutumika kwa ajili ya  kubeba wagonjwa

waziri pinda akiwasili  katika jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha

  Waziri mkuu akielekea kukabidhi rasmi magari mawili ya kubebea wagonjwa 

mkuu wa mkoa wa Arusha akiongeozana na waziri mkuu kwa ajili ya makabidhiano ya magari ya kubebea wagonjwa yaliyoletwa na waziri


Habari picha na Woinde Shizza,Arusha


Waziri Mkuu  wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda leo  amekabithi magari mawili  ya kubebea  wagonjwa yenye dhamani ya shilingi milioni 150.

Magari hayo ambayo yamekabidhiwa, yametokana na ahadi ambayo waziri huyo alitoa Kwa Wananchi wa wilaya ya ngorongoro wakati Alipofanya ziara wilaya ni humo september 2013.

Akizungumza wakati akikabidhi magari hayo waziri mkuu Mizengo Pinda  alisema wakati alipokuwa kwenye ziara wilaya ni humo, alipokea malalamiko ya kutakuwepo na magari ya kubebea  wagonjwa hali ambayo ili mfanya atoe ahadi nasasa ameamua kuitekeleza.

"nilipata malalamiko nikapeleka wizara ya afya, wakapokea na kaniambia watafanyia kazi sasa Kila  nikiwauliza Wakaniambia bado sasa nikabahatika kupata safari ya Kwenda japani nilipoenda Nitakuja na na Wananchi wa Tanzania wa naishi uko nikawaomba wa nisaidie japo gari moja ya kubebea wagonjwa sasa wao  ndio wakaja wakanipa magari haya mawili "alisema pinda

Alisema Kuwa mara baada ya kupokea magari hayo aliyafanyia ukarabati mdogo na sasa ameamua kuyaleta Mkoani ili yapelekwe katika wilaya husika ambapo alisema Kuwa mara baada ya kufikishwa wilaya ni ngorongoro  gari moja litatumika katika hospitali ya waso huku ingene ikitumika hospitali ya Enduleni.

Aidha aliwataka viongozi wa wilaya ya ngorongoro kutumia vyema magari hayo haswa katika shughuli iliolegwa, Pamoja na kuyatunza ili ya weze kutumika na kubeba wagonjwa wakati Mgonjwa anapotokea au tatizo la gafula linapotokea.

Aidha alibainisha Kuwa magari haya ameyatoa yeye mwenyewe  kutoka Kwa wa fadhili na sio magari ya wizara hivyo wakapokee haya wakijua ni ahadi ya waziri  mkuu, na sio ya wizara hivyo wapokee haya wakati wakiwa Wana ngoja magari ya kubebea wagonjwa kutoka wizarani


Alipokea msaada huo mkuu wa wilaya ya ngorongoro Ashimu Mgandila alisema Kuwa wa nashukuru sana Kwa msaada hii kwani Wananchi haswa wakina mama waja wa zito wali Kuwa wanateseka sana wakati walipo Kuwa wa naumwa.

Alisema  Kuwa wali Kuwa na gari ya kubebea  wagonjwa lakini imearibika Kwa kipindi karefu ila hii itakuwa ni suluisho Kwa Wananchi wa wilaya hiyo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ngorongoro  John kulwa alisema Kuwa magari  haya ni ukumbozi hasa Kwa upande wa wamama Pamoja na wagonjwa mahututi kutaka katika Kila kata na Kila kaya.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO