Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

ZIARA YA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA MKOANI MOROGORO

 

Mgombea urais kupitia vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Mh Edward Lowassa amesema hakuna sababu ya wamiliki wa viwanda vya sukari kuendelea kuwaumiza wakulima na endapo atapata ridhaa ya watanzania atahakikisha anarudisha kiwanda cha Mtibwa mikononi mwa wananchi na atasimamia kuhakikisha jasho la wakulima wa miwa halipotei bure.

Mh.Lowassa akizungumza na umati mkubwa wa wananchi wa mji wa Dumila na Turiani wilayani Mvomero alikoanzia mikutano yake amesema kwa nafsi yake anaumizwa na hali ya wakulima wa miwa kukopwa jasho lao bila kulipwa na endapo atapata ridhaa atahakikisha kilimo kinawainua wakulima na hakuna sababu ya wakulima wa miwa kushindwa kunufaika na viwanda vinavyowazunguka huku wawekezaji wakiendeelea kuneemeka na atahakikisha kiwanda cha Mtibwa kinarudi katika mikono ya wananchi na kufuta ushuru wa mazao na mifugo.

Katika mkutano wa mjini Morogoro uliofanyika katika viwanja vya Sabasaba Mh Lowassa akizungumza na maelfu kwa maelfu ya wananchi wa mji wa Morogoro wakiwemo waliokesha katika uwanja huo kusubiri kusikia sera za mabadilko ambapo Mh Lowassa amesema akipata ridhaa hatowaangusha wananchi kwakua amedhamiria kuhakikisha nchi anamaliza matabaka ya wenye nacho na wasiokuwa nacho fursa za ajira na kufufua viwanda.

Nae alikuwa waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akizungumza na wananchi hao amesema wananchi wamesubiri sana na sasa wanataka mabadikio kutokana na ahadi zisizotekelezeka ikiwemo huduma za elimu na kuwataka wananchi kufanya maamuzi magumu kwa kuchagua Lowassa ili akasimamia rasilimali za nchi zinufaishe wananchi.

Wagombea ubunge wa jimbo la Mvomero Mh Osward Mlay na mgombea ubunge jimbo la Morogoro mjini Marcus Albanus wakizungumza kwenye mkutano wamesema mabadiliko wanayoyataka wananchi ni sasa hivi ni kuondoa kero zilizoshindikana kwa miaka mingi ikiwemo kero ya maji hospitali kukosa madawa pamoja na kufufua viwanda 14 vya mji wa Morogoro vilivyokufa baada ya kupewa wawekezaji hali inayosababsiha wanwake na vijana kukosa ajira.

Baada ya mchakamchaka uliovunja rekodi ya kuwana wananchi wengi mjini Morogoro Mh Lowassa kesho anatarajia kuendelea kunadi sera za mabadiliko katika mkoa wa Simuyu.

CHANZO: CHADEMA BLOG

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO