Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MWANAKOTIDE WA CHADEMA NA WENZAKE WAPANDISHWA KIZIMBANI NA KUACHIWA KWA DHAMANA DODOMA

mwanakotide

Mwanakotide na wanachama wenzake watatu wa CHADEMA walipandishwa kizimbani jana Mjini Dodoma katika Mahakama ya Wilaya na kusomewa mshitaka nane na mwansheria wa Serikali  Beatrice Nsana ya shambulio la kudhuru mwili na uharibifu wa mali za CCM mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi James Karayemala.

Wanachama hao ambao walikuwa mjini Dodoma kwa shughuli za Kurugenzi ya Sanaa za chama hicho, wakiongozwa na mtunzi namwimbaji mahiri wa wimbo maarufu wa “chadema…Chadema..Peoples Power..” Bw Fulgence Mapunda almaarufu kama Mwanakotide wameyakana mashtaka hayo. Wengine pamoja nae ni Juma Bika, George Mwingira na Deogratius Peter.

Hata hivyo vijana hao wanaotetewa na Wakili Fred Kalonga wameachiwa huru kwa dhamana na kesi yao itatajwa tena Oktoba 5, 2015.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO