‘Cardiac Arrhythmia’ ni pale mtu anapokuwa na mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida au yanayodunda sana. Mwili una mfumo asili wa umeme unaosaidia moyo kufanya kazi. Mfumo huu husababisha moyo kutanuka na kusinyaa ambapo husababisha damu kuingia na kutoka kwenye moyo; umeme kwa kawaida hufuata mkondo na mapigo ya moyo kwa kasi ya kawaida. Ingawa, kama mkondo wa kawaida wa umeme huu ukivurugwa moyo hushindwa kufanya kazi na kusababisha mapigo ya moyo ama kwenda taratibu sana, haraka sana au yasiyoimara.
Kuna aina kadhaa za ‘Arrhythmia’; Baadhi ni pamoja na zijulikanazo kitaalamu kama Supra-Ventricular Tachycardia, Ventricular Tachycardia, Ventricular Fibrillation, Atrial flutter and Atrial Fibrillation.
Mapigo ya moyo yasiyo imara hasa husababishwa na ugonjwa wa moyo na moyo kushindwa kufanya kazi. ‘Arrhythmia’ ndogo pia huweza kusababishwa na mtindo wa maisha usiozingatia afya bora ikiwa ni pamoja na uvutaji sigara uliopitiliza, Ulevi na kuzidisha matumizi ya kafeini au msongo wa mawazo.
Ingawa imegundulika hasa katika uchunguzi wa mara kwa mara wa matibabu dalili za ‘arrhythmia’ ni chache zinazoweza kuonekana ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo, kupungua kwa mapigo ya moyo, maumivu ya kifua, kizunguzungu, kuchoka sana na kukosa pumzi.
‘Arrhythmia’ mara nyingi hutokea kwa nyakati tofauti tofauti. Hali ya kutotabiri kwa ‘arrhythmia’ na kutokea kwake kwa nyakati tofauti tofauti hufanya uchunguzi kuwa mgumu. Moja ya vifaa vitumikavyo zaidi kwa uchunguzi wake kitaalamu ni ‘electrophysiology (EP)’ na kinachukuliwa kuwa bora zaidi katika taaluma hii.
Utafiti wa EP hufanya kazi kwa kupima na kurekodi shughuli za umeme wa moyo na kuonesha njia za umeme. Inaonesha sababu na mahala penye tatizo la mapigo ya moyo. Matatizo yanayotokea katika utafiti wa EP ni machache sana kwa kuwa umekuwa ukifanyika salama kwa miaka mingi sasa.
Taarifa inaweza kuundwa katika namna mbili, ama kupitia ramani ya shughuli za umeme wa moyo kupitia kifaa maalumu kitaalamu ‘electrocardiogram (ECG)’ inayoonesha wapi ishara zisiyo za kawaida zinaanza kutokea ndani ya moyo.
Mfumo wa wa kitaalamu wa ‘Carto3’ ujulikanao kama ‘3D mapping’ ni teknolojia mpya inayotoa muonekano wa moyo kwa ukubwa mara tatu zaidi. Hii hupelekea kuboreshwa kwa usahihi wa vipimo na matibabu ya mgonjwa.
Kwa kesi ya kushuka kwa mapigo ya moyo, utafiti wa EP unatoa nafasi kutathmini haja ya vifaa kama vile ‘peacemaker’ au ‘defibrillator’ ambavyo husaidia kuzuia vifo vya ghafla vya magonjwa ya moyo.
Baada ya uchunguzi kupitia utafiti wa EP, mirija maalum ya ‘Radiofrequency (RF) catheter ablation’ huingizwa katika mishipa ya damu ambapo viwango vya juu na vya chini vya mzunguko wa nguvu ya umeme vinapokelewa katika tishu za moyo na kuharibu tishu zile zinazohusika na mapigo ya moyo ‘arrhythmia’. Baada ya matibabu kwa kawaida wagonjwa sasa huweza kikamilifu kupunguza matumizi ya dawa ambapo mgonjwa ataweza kupumua vizuri na mapigo ya moyo kwenda vizuri.
kwa mujibu wa Dkt A M Karthigesan wa hospitali za Apollo baadhi ya ‘arrthythmia’ zilitibiwa kupitia kipimo maalumu kijulikanacho kitaalamu kama ‘RF Ablation’ ni ‘Supraventrical Tachycardia (SVT’; hii inatokea kwenye vyumba vya juu vya moyo na kwa ujumla inaelezewa kama moyo kupiga kwa kasi. Pingili za ‘Atirioventrikali (AVNRT)’, ‘atirioventrikali reentry (AVRT)’ na ‘focal atrial tachycardia’ ni baadhi ya aina nyingi za SVT.
Zaidi ‘Atrial Flutter (AFL)’ inaweza pia kutibiwa kwa upasuaji wa RF. AFL ni wakati atria inapopiga haraka sana kwa kiwango cha karibu mapigo 300 kwa dakika yanayotokea katika chumba cha juu cha moyo.
Arrhythmia nyingine maarufu inayotibiwa kwa RF ni ‘Atrial Fibrillation (AF)’. Hii ni wakati uwezo wa moyo kufanya kazi zake unapunguzwa kwa mapigo yasiyo na mpangilio ya chumba cha juu cha moyo. Ingawa ‘atrial fibrillation’ haitishii maisha, kuongezeka kwa mapigo ya moyo huweza kupelekea matatizo kama vile damu kuganda ambapo hatimaye inaweza kusababisha kiharusi.
Mwisho ‘Ventricular Tachycardia (VT)’ ambayo kama ikiachwa bila kutibiwa inaweza kuwa aina ya ‘Arrhythmia’ ya kuhatarisha maisha, hii hutokea wakati chumba cha chini cha moyo kikimpiga kwa kasi sana
Dkt. A M Karthigesan wa hospitali za Apollo anasema kuwa baadhi ya manufaa ya kufanyiwa tiba ya upasuaji kwa mirija ni kuwa mtu atarajie mabadiliko ya haraka katika ubora wa maisha sababu ya kuongezeka kwa uwezo wake wa kufanya kazi; Huduma ya matibabu iliyoboreshwa kwa jinsi mgonjwa anavyohitaji imeondoa upotevu wa muda; Kupungua kwa gharama za tiba na kuokoa maisha ambapo mgonjwa anapewa nafasi nyingine ya kuishi.
Imechangiwa na:
Dkt A M Karthigesan
Mshauri wa tiba ya umeme wa moyo
Hospitali za Apollo, Chennai
0 maoni:
Post a Comment