Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

EKARI 7000 KUGAIWA KWA WANANCHI WA ARUSHA.

shamba

 

Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Serikali imetwaa jumla ya Ekari 7000 baada ya ubatilishwaji wa Mashamba ya Tanzania plantatition limited yaliyokua yakimilikiwa na mwekezaji kutoka nje ,mashamba hayo yanatajiwa kugawanywa kwa wananchi 2000 wenye uhitaji wa ardhi ya makazi na mashamba .

Aidha baada ya ubatilishwaji wa mashamba hayo Arusha imepata ekari 6176.5 na Halmashauri ya Meru ekari 925 hivyo kufikia ekari 7101 ambazo zitagawanywa kwa wananchi.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi,Wiliam Lukuvi wakati akitoa taarifa ya usuluhishi wa migogoro ya ardhi katika mikoa ya Arusha na Manyara katika mkutano wake na Waandishi wa Habari,Lukuvi amesema kuwa mashamba hayo yalikua na migogoro kwa kipindi kirefu kati ya mwekezaji na Wananchi hivyo kutokana na uhitaji mkubwa wa ardhi serikali imeamua kubatilisha mashamba hayo.

“Nimekuja Arusha na timu yangu ambayo itafanya uhakikiki wa watu 2000 wenye uhitaji na baada ya kujiridhisha watafanya zoezi la ugawaji na pia wananchi watapatiwa hati ya kumiliki ardhi zao safari hii hatutagawa ardhi kienyegi” Alisema Lukuvi

Lukuvi amesema kuwa mbali na shamba hilo pia wamepata ekari 100 katika shamba la Imani Estate na pia Shamba la Noors lenye Ekari 2296 lililokua na mgogoro kati ya Mwekezaji na wananchi wa Kijiji cha Laroi na Kisima cha Mungu litagaiwa kwa wananchi baada ya mazungumzo kati ya Mwekezaji kukubali kuachia shamba hilo

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha DC ,Fidelis Lumato amesema kuwa ugawanywaji wa mashamba hayo utasaidia kupunguza migogoro mikubwa ya ardhi iliyokua inakabili wilaya hiyo kutokana na uhaba mkubwa wa ardhi.

Jumla ya migogoro 80 iliyowasilishwa kwa Waziri Lukuvi kutoka katika Halmashauri ya Jiji la Arusha ,Halmashauri ya Wilaya ya Arusha na Halmashauri ya Meru imepatiwa ufumbuzi hivyo kupunguza migogoro ya ardhi ilikua ikilisakama jiji la Arusha

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO