Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MARUFUKU KUBEBA MAJENEZA KWENYE KAMPENI ZA KISIASA MKOANI ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw Daudi Felix Ntibenda

Ubebaji majeneza kabika shamshamraCarrying coffins to prophesy demise of any political party has been banned in Arusha  by local authorities.

Wakati kipyenga cha kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu baadae mwezi Oktoba mwaka huu kikiwa kimeshapulizwa, mashabiki na wafuasi wa vyama vya siasa wametahadharishwa kutotengeneza majeneza na vinyago vya kudhihaki ama kuzodoa vyama vingine. Vitu vya aina hiyo vimepigwa marufuku kwa maeneo yote ya Mkoa wa Arusha na sio mjini pekee.

Mratibu wa Uchaguzi Arusha, Bw Richard Kwitega ameyasema hayo katika mkutano wa hivi karibuni na wawakilishi wa vyama vya siasa vilivyoko mkoani hapa. Marufukku hii inahusu kampeni kwa ngazi zote kuanzia udiwani, ubunge hadi urais.

Katika kampeni zilizopita imeshuhudiwa baadhi ya mashabiki wa vyama vya siasa wakitengeneza mfano wa majeneza kumaanisha kuzika vyama vingine, na wengine wakiendaa mbali zaidi na kutengeneza vinyago vyenye sura za watu wengine wanaowakebehi.

Marufuku hiyo inahusu hata matumizi mabaya ya bendera za vyama vingine na kuzitumia kufanyia matendo yanayofanania na dhihaka, pmaoja na kutofanya matangazo ya mikutano ya kisiasa zaidi ya saa kumi na mbili jioni.  

Katika hatua nyingine Tume ya Elimu Mkoani hapa imevizuia vyama vya siasa kutotumia viwanja vya shule kwa ajili ya kampeni kwasababu kumekuwapo na matukio ya uharibifu wa mali za umma, a hivyo kuwashauri wafanyie mikutano yao mahali kwingine.

Katika kuhiimisha, Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliwataka wananchi wa Arusha kuheshimu sheria wakati wote na sio tu wakati huu wa kampeni.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO