Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MKE HALALI WA NDOA WA DK.WILBROD SLAA, MBUNGE ROSE KAMILI AMLIPUA DR SLAA

 

Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chadema,Rose Kamili,akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo jioni kuhusiana na tuhuma alizozitoa mume wake kwamba waliishi kwa maisha ya kula mihogo na familia yake ili kuhakikisha chadema inastawi na kuimarika jambo ambalo si la kweli walikuwa na maisha mazuri ya kawaida tu na kusema kuwa Dk.Slaa anapaswa awaombe radhi wataznzania kwa kufafanisha kula mihogo kuwa ni umaskini na kuongeza kwa kusema mbona ukienda katika mahoteli makubwa mihogo na viazi ipo na watu wenye pesa zao wanakula kama kawada.

akizungumzuia kuhusu matamshi aliyasema Dk.Slaa kwamba haongei na waziri mkuu mstaafu,Sumaye,mama rose kamili alisema kuwa wiki tatu zilizopita waziri mkuu huyo mstaafu aliomba namba za dk.slaa akampatia wakaongea vizuri bila shida yoyote ila anamshangaa juzi aliposema mbele ya waandishi wa habari kwamba hazungumzi na sumaye.

akizungumzia kuhusu kuja kwa lowassa chadema mama huyo alisema kuwa Dk.slaa alikuwepo katika kumkaribisha waziri mkuu mstaafu,Edward Lowassa kujiunga na chama hicho ni jambo la kushangaza akizungumza kwamba hakushiriki na pia wakati chokochoko hizo za kustaafu ukatibu wake alisema kuwa viongozi waandamizi wa chama cha mapinduzi walimfuata na kumshawishi kutoludi kwenye ukatibu mkuu wake huo atapewa ubunge wa kuteuliwa na rais atakayeapishwa na kupewa uwaziri katika serikali ya awamu ya tano.


Kamili alimaliza kwa kutoa rai kwa watanzania wote nchini kutomsikiliza Dk.Wilbrod Slaa na kuwasihi kuendelea kuwa na matumaini na mgombea wa urais wa Chadema,Edward Lowassa aliyesimamishwa na chama chao pamoja na umoja wa katiba ya wananchi (Ukawa) ili kukiondoa madarakani chama tawala.

Linus Slaa.

Emiliana Slaa.

Mama Rose Kamili akizungumza kwa hisia kali.kushoto ni mtoto wake aliyezaa na Dk.Slaa aitwaye,Emiliana Slaa.

Mama Rose Kamili akizungumza kwa hisia kali.kulia ni mtoto wake, Linus Slaa.

waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini leo

Mbunge wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Rose Kamili, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya mume wake Dk.Wilbrod Slaa kuzungumza wakati akiwa Katibu mkuu wa chadema familia yake ilikula kwa shida kwa sababu ya kujenga chama hicho jambo ambalo si la kweli. Wengineo ni watoto wake, Linus Slaa (kulia) na Emiliana Slaa.

CHANZO:HABARI TANZANIA

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO