Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Godbless Lema na Wenzake Waachiwa Kwa Dhamana, Alikamatwa Tangu Jana Jioni Baada ya Mkutano wa Kuzindua Kampeni za CHADEMA Arusha

LEMA2
Lema akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuachiwa huru.
****

Imeandikwa Na Sauli Giliard, Mwananchi

Mgombea ubunge jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema na wenzake wanne wameachiliwa kwa dhamana leo baada ya kushikiliwa na polisi tangu jana.

Polisi mkoani Arusha walimkamata mwanasiasa huyo pamoja na watu wengine wanne jana jioni mara baada ya kuzindua kampeni yake ya kuwania ubunge katika jimbo hilo kwa awamu ya pili katika Shule ya Msingi Ngarenaro.

Wakisomewa mashtaka katika mahakama ya Arusha, Lema amedaiwa kulizima gari lake wakati wakitokea kwenye mkutano wa kampeni, hali iliyowafanya wafuasi wake kuanza kulisukuma hivyo kusababisha maandamano pasipo kuwa na kibali cha polisi. Lema na wenzake wameyakana mashtaka dhidi yao.

Mwanasiasa huyo na wenzake wameachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana waliyowekewa.

LEMA
Mh Lema akitoa maelezo Kituo Kikuu cha Polisi Arusha
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO