Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

IJUE HISTORIA YA FREEMAN AIKAEL MBOWE NA MAGEUZI

MJUE FREEMAN AIKAEL MBOWE
FREEMAN AIKAEL MBOWE
Freeman Aikael Mbowe alizaliwa tarehe 14/09/1961 Wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro.
Mbowe ni miongoni mwa Watu waliofanya Kazi katika Bank kuu ya Tanzania kama Afisa wa Bank Kuu (BoT)  akiwa chini ya Edwin Mtei, Bob Makani.

Katika harakati za kisiasa, Freeman Aikael Mbowe aliingia rasmi katika siasa mwaka 1992.
Freeman Aikael Mbowe ni miongoni mwa WAASISI au waanzilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) chama ambacho kilisajiliwa usajili wa kudumu mwaka 1993 kwa namba 0000003 kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu cha 7(1),(2),(3), kifungu cha 8(1),(2),(3)(4)& (5)pamoja na kifungu cha 9(1)(a)(b)(c) (2)(a),(b),(c),(d),(e) na 10(1)(a),(b),(c) na (d)
Mbowe akiwa ndio kijana mdogo kuliko Wote wakati wa uasisi wa CHADEMA aliingoza kurugenzi ya Vijana ya CHADEMA chini ya Uenyekiti wa Edwin Mtei. Waasisi wengine wa CHADEMA kutaja kwa uchache ni Pamoja na -
1/EDWINI MTEI - ARUSHA
2/BOB MAKANI - SHINYANGA
3/FREEMAN MBOWE - KILIMANJARO
4/BROWN NGWILUPIPI - MBEYA
5/EDWARD BARONGO - KAGERA
6/WASIRA-MARA
7/MENRAD MTUNGI - KAGERA
8/MARRY KABIGI-MBEYA
9/EVARIST MAEMBE - MOROGORO
10/COSTA SHIGANYA - KIGOMA

Wakati wa kusaka wanachama wa CHADEMA ili kupata usajili wa Muda(Provisional registration) kwa mujibu wa sheria ya vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu cha 8 na usajili wa kudumu (Full registration) kwa mujibu wa kifungu cha 10(1)(b) kinachotaka chama cha siasa Ili kupata usajili wa kudumu ni lazima kiwe na wanachama miambili katika mikoa kumi(10) huku mikoa miwili ikiwa mmoja Pemba na mwingine Unguja, CHADEMA iliasisi hatua hiyo kama SAFARI YA TREN KUTOKA DAR ES SALAAM KWENDA KIGOMA.

Dhana ya "SAFARI YA KUTOKA DAR ES SALAAM KWENDA KIGOMA ilimaanisha kwamba, katika dhamira ya kutafuta mabadiliko ya kweli na kuunda Serikali kwa kushinda uchaguzi , wapo watakaonunuliwa, wapo watakaoamua kuacha siasa, wapo watakaohama chama, wapo watakaoachana na CCM na kupanda Treni popote iwe Morogoro, Dodoma, Kibaha nk.

Kwa tafsiri nyepesi, Mbowe na Waasisi wenzake waliipa safari ya kutoka Dar Es Salaam kwenda Kigoma kwamba kufika Kigoma ni CHADEMA kushinda uchaguzi na kuunda serikali. Waliamini kwamba katika safari, wengine watashukia Kibaha, wengine watapanda, wengine watapanda Treni Morogoro, wengine watashuka, wengine watapanda Dodoma wengine watashuka. 

Hivyo walimaanisha kwamba, katika safari ndefu ya kufika kigoma (Kipindi hicho safari ya Treni kutoka Dar Es Salaam kwenda Kigoma ilikua ni ya shida, mteso na maumivu. Ilichukua siku Tatu hadi Tano kutoka Dar Es Salaam kufika Kigoma.). Hivyo Mateso waliyoyapata Waasisi kuijenga CHADEMA walifananisha na safari ya kutoka Dar Es Salaam kwenda Kigoma. Mfano, Viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Edwin Mtei, Bob Makani, Freeman Mbowe, Mary Kabongo na Evarist Maembe walipigwa mawe na kufukuzwa na wananchi Morogoro. Waliambiwa kwamba CHADEMA ndio nini?? Kwa nini mnampinga chama chetu kilichotukomboa Kutoka kwa utumwa wa wakoloni. Kwa nini mnapinga chama cha Mwalimu Nyerere baba wa taifa ??.Kwa nini mnapinga chama cha wanyonge CCM chama chenye matumaini kwa wakulima na wafanyakazi????. Waasisi hawa walipigwa mawe, kufukuzwa maeneo mbalimbali, kutukanwa, kudhalilishwa na kudhihakiwa. Kuzungumza siasa za upinzani ilionekana ni usaliti, uhaini nk. Yote hayo, walivumilia. Wengine walikata tamaa,wengine waliamua kurudi Ccm, wengine waliamua kulinda Vyeo vyao na maslahi yao na kurudi Ccm.

Mwaka 1995 Edwin Mtei na Bob Makani wote wawili walichukua Fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wote walionekana kuwa na nguvu. Mapambano huo ulileta sitofahamu kubwa ndani ya CHADEMA. Freeman Mbowe kama kijana alitoa ushauri kwa chama kwamba CHADEMA isisisimamishe mgombea urais ili kuepusha mpasuko ndani ya chama na badala yake CHADEMA imuunge mkono mgombea wa urais kupitia NCCR MAGEUZI Agustine Lyatonga Mrema. Ushauri huu wa Mbowe uliungwa Mkono na wanachama na Viongozi. Mtei na  Makani waliacha mchakato huo na CHADEMA ilimuunga mkono mgombea urais Lyatonga Mrema.

Freeman Aikael Mbowe alichukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Hai mwaka 1995. Mbowe wakati wa Kampeni jimbo la Hai , aliombwa kugharamia Mkutano wa mgombea urais Lyatonga Mrema na aliahidiwa kwamba Mrema atamnadi jukwaani. Mbowe kwa kuwa alikua na Fedha na uchumi mzuri, aligharamia Mkutano na malazi ya timu ya kampeni ya Mrema nk. Lakini Mrema alipofika Jukwaani alimpuuza Freeman Mbowe wa CHADEMA na kumnadi mgombea wa NCCR MAGEUZI aliyeitwa Mwinyihamisi Mushi. Katika uchaguzi huo Mgombea wa NCCR MAGEUZI Mwanahamisi Mushi alishinda uchafu kwa kupata kura 29,046 (52.0%) huku Freeman Mbowe akiambulia kura 15,995(28.6%)

Mbowe hakukata tamaa, Mwaka 2000,Freeman Aikael Mbowe aligombea tena ubunge jimbo la Hai na kupata ushindi mnono wa kura 64.5% dhidi ya mpinzani wake wa NCCR MAGEUZI ambaye alipata mweleka kutokana na chama chake kuwa na mvurugiko mkubwa ndani ya Chama kutokana na mgogoro mkubwa wa kisiasa kati ya Mabere Nyaucho Marando  na Agustine Lyatonga Mrema. Mbowe aliongoza jimbo la Hai mpaka mwaka 2005.

Katika nafasi ya Urais, Mbowe na CHADEMA Kwa ujumla walikubaliana kwamba CHADEMA isisimamishe mgombea yeyote bali chama kimuunge mkono mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof Ibrahim Haruna Lipumba.

Mwaka 2004,Freeman Mbowe aligombea uenyekiti wa CHADEMA TAIFA na kushinda akimpokea Bob Makani ambaye aliongoza kuanzia mwaka 1999. Mbowe baada ya kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA alifanya mabadiliko makubwa Sana ndani ya chama.

Baada ya kuchaguliwa, Mbowe alifanya mabadiliko makubwa Sana Ni kipindi hiki Mbowe alianza kutembelea vyuo vikuu mbalimbali vya Tanzania, kufuatilia wanasiasa mbalimbali kutoka CCM, NCCR MAGEUZI, CUF, TLP na vyama vinginevyo. Mifano iko Mingi.

John Mnyika ambaye alikua mwanaharakati wa kutetea haki za wanafunzi na watu mbalimbali na pia akiwa mtangazaji wa Redio One Stereo, Freeman Mbowe alimshawishi kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kuungana na wanamabadiliko wengine. Hata hivyo, UWEZO mkubwa wa John Mnyika ambao aliuonesha katika ukumbi wa Nkrumah Chuo kikuu cha Dar Es Salaam (ingawa yeye alikua akisoma masomo ya jioni) alisimama na kupinga sera ya uchangiaji wa masomo elimu ya Juu (cost sharing) na kusababisha wanafunzi kuanza Mgomo chuoni hapo. Mnyika akiwa Morogoro, aliombwa kutuliza hali hiyo na alipofika chuoni, aliita wanafunzi na kuwaambia mambo kadhaa ili kupima ujasiri wao. Alimuomba Rafiki yake kurusha jiwe katikati ya kusanyiko Mabibo Hostel, baada ya kurushwa jiwe Hilo, wanafunzi walitawanyika kukimbia ndipo Mnyika akasema ninyi ni waoga. Hamuwezi kupambana. Nawataka muache Mgomo endeleeni na masomo.

Mnyika alikua mfuasi wa CHADEMA tu mpaka 2005 alipoamua kujiunga rasimi CHADEMA na kuchukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Ubungo. Alipochukua fomu ya Ubunge, Chuo kikuu cha Dar Es Salaam kilimfukuza kama njia ya kumdhoofisha. Mbowe alipoona uwezo wa Mnyika wa hoja, umakini, weledi na akili Alimuomba kujiunga na CHADEMA. Hotuba ya John Mnyika Bungeni mwaka 2001 akielezea kuhusu UONEVU na uharibifu wa Serikali baada ya kumuua mwanafunz mmoja Kule shule ya Sekondari Iyunga Mbeya ni rekodi pia kubwa kwa Mnyika.

Mbowe pia alifanikiwa kumvua samaki nguli wa siasa Zitto Zuberi Kabwe (ZZK) akiwa ni kiongozi chuo kikuu cha Dar Es Salaam. Zitto Kabwe akiwa Waziri mkuu wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam na mwanaharakati wa utetezi wa wanafunzi (moja ya WAASISI wa TSNP) alifanikiwa kuvuliwa na Mbowe. Mbowe alimshuhudia Zitto Kabwe katika majukwaa ya chuo kikuu cha Dar Es Salaam hasa mahali maarufu kama REVOLUTION SQUARE. Zitto alionekana kutoa matamko mbalimbali yaliyoitetemesha Serikali akihoji Ufisadi, kuibua uchafu mbalimbali wa Serikali ya Mkapa, na pia utetezi wa wanafunzi. Mbowe alimuona Zitto na kushawishi ajiunge CHADEMA. 

Zitto Kabwe alikubali kujiunga CHADEMA na Mwaka 2005 Zitto Kabwe aligombea ubunge jimbo la Kigoma Kaskazini na alinadiwa na Freeman Mbowe kama mgombea urais wa CHADEMA. Zitto Kabwe alishinda jimbo hilo na kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Halma James Mdee naye ni miongoni vijana ambao Mbowe aliweza kuwashawishi kuingia katika siasa. Zitto na Halma Mdee wakiwa marafiki Sana chuoni, Halma Mdee akisomea Sheria na Zitto akisomea Uchumi, kama iliyokua kwa Zitto, Halma Mdee kama mwanaharakati wa Kutetea wanafunzi (Muasisi wa TSNP) alikubali kujiunga na CHADEMA.

Tundu Antipas Lissu ambaye alikua mwanachama wa NCCR MAGEUZI pia alifuatwa na Freeman Mbowe kuomba msaada wake katika mambo ya Sheria kutetea wanachama wa CHADEMA, wananchi katika migodi mbalimbali nk. Tundu Lissu alikua ni tishio kubwa katika mambo ya Sheria na mtetezi mambo ya mazingira. Alipinga na kupambana vikali Sana na serikali ya Benjamin Mkapa iliyowapa wawekezaji migodi na kufukuza wananchi maeneo mbalimbali ya nchi hasa Geita, Shinyanga, Mara nk. Harakati hizi za Lissu ziliifanya Serikali ya Mkapa kumtafuta na baadaye Lissu alielekea Uingereza na baadaye Afrika Kusini. Kutokana na rekodi hiyo ya harakati za mapambano, Freeman Mbowe alimuona Lissu ni silaha nzuri dhidi ya Ccm na silaha njema katika ukombozi wa Mtanzania. Alimuomba kujiunga CHADEMA.

Wengine waliojiunga na CHADEMA kipindi cha uongozi wa Mbowe kuanzia mwaka 2004 ni Pamoja na Prof Mwesigwa Baregu, Livingstone Lusinde (alirudi Ccm na sasa ni Mbunge wa Mtera), Peter Msigwa kutoka TLP, David Ernest Silinde na wengine wengi. Ni kipindi hiki CHADEMA ilifungua milango kwa wanachama kujiunga, Wasomi na vijana walijiunga CHADEMA. Baadhi ya watu walianza kuita CHADEMA ni Chama cha vijana Wasomi ingawa hata wazee Wasomi walijiunga.

Mabadiliko mengine aliyotaka Mbowe ni Pamoja na kutumia ngumi kama ishara ya salamu ya chama
Mwaka 2005 Freeman Mbowe  aligombea uraurais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa na mgombea mwenza kutoka Zanzibar bwana Jumbe Rajab Jumbe ambaye alifariki siku chache kabla ya uchaguzi mkuu uliokua ufanyike tarehe 30/10/2005 na hivyo uchaguzi kuahirishwa mpaka tarehe 14 /12/2005.

CHADEMA ilimteua mgombea mwenza Anna Maulid Komu kuwa mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika uchaguzi ule, Mbowe alitumia chopper au Helkopta kupiga kampeni maeneo mbalimbali nchini na kubatizwa jina "Kamanda wa Anga".Katika kampeni za urais Mbowe aliasisi Vazi la Magwanda ya Khaki na neno Kamanda kwa mwanachama yeyote wa CHADEMA .

Wakati wa kampeni, Mbowe alipendelea kuvaa Nguo za khaki zenye sura ya gwanda kwa kuwa zilikuwa hazichafuki Sana na Muda wa kufua mara kwa mara haukuwepo. Alipofika eneo fulani kwa ajili ya kampeni za urais, wananchi walimshangilia na kumwambia kwamba amependeza Sana kuvaa zile nguo za kikamanda(Magwanda ya khaki). Aliwauliza wananchi, niendelee kuvaa mavazi ya kikamanda?? Maelfu ya wananchi wakajibu ndio oooooooo oooooooo. Mbowe akawaahidi wananchi kwamba atapeleka pendekezo kamati kuu, Baraza kuu na Mkutano mkuu ili gwanda la khaki kuwa Vazi rasimi la Kamanda wa CHADEMA (mwanachama wa CHADEMA).Mbowe alifikisha pendekezo hilo kamati kuu ya CHADEMA baadaye Baraza kuu na kupitishwa na Mkutano mkuu 2006 kuwa Vazi rasimi la chama.

Jakaya Mrisho Kikwete alishinda kwa kishindo uchaguzi mkuu ule kwa kupata ushindi wa 80.28% akifuatiwa na Prof Haruna Ibrahim Lipumba aliyepata 11.68% na Freeman Mbowe akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 5.88%.

Miaka ya 2008,2009 CHADEMA chini ya Mbowe ilishiriki chaguzi ndogo ambazo ni Pamoja na Uchaguzi wa Jimbo la Busanda, Jimbo la Tarime na Mbeya vijijini. CHADEMA ilishinda Tarime na kushindwa Busanda huku jimbo la Mbeya vijijini Shambwee Shitambala alijiapisha kupitia ofisi yake ya Mawakili hali iliyopelekea CCM kupitia mgombea wao Luckson Mwanjali kuweka pingamizi dhidi ya Shitambala na hivyo CCM kupata ushindi dhidi ya wagombea dhaifu wa TADEA, TLP nk.
Mwaka 2009, Freeman Mbowe aligombea tena uenyekiti wa CHADEMA. Alipata mpinzani Zitto Zuberi Kabwe. 

Zitto alitangaza kugombea uenyekiti wa CHADEMA taifa na kutoa sababu zake za kutaka nafasi hiyo katika gazeti la The Citizen la tarehe 26/08/2009. Zitto alieleza kwamba anaweza kuisaidia CHADEMA kushinda serikali za mitaa 2009 na uchaguzi mkuu 2010.Wazee wa CHADEMA walimuomba Zitto Kabwe kujitoa kugombea ili Freeman Mbowe kupita bila Kupingwa. Jambo hili liliwaumiza Sana wafuasi wa Zitto Kabwe akiwepo Habib Mchange, David Kafulila, Mtemelwa, Nyakarungu, Mtela Mwampamba nk.

Katika uongozi wa Freeman Mbowe mwaka 2004-2010 ilifanyika Operation maarufu Sana "OPERATION SANGARA KANDA YA ZIWA " ambayo ilihusisha Katibu Mkuu Dk Slaa, John Mnyika kama mkurugenzi wa vijana, Zitto Kabwe na Viongozi mbalimbali.

Operation Sangara ilisababisha CHADEMA kuungwa mkono na kupata wabunge wengi Kanda ya ziwa katika majimbo ya Maswa Magharibi, Maswa Mashariki, Bukombe,Ukerewe Musoma mjini, Nyamagana, Ilemela,na majimbo mengine mengi mikoa ya Kagera, Shinyanga, Mwanza
Baada ya Mbowe Kushinda tena kama Mwenyekiti wa CHADEMA (Kupita bila Kupingwa) mwaka 2009 aliongoza chama katika uchaguzi mkuu mwaka 2010 ambapo yeye aligombea tena ubunge jimbo la Hai na kupata kura 28,545(51.63%) huku mgombea wa CCM Godwin Kimbita akipata kura 23,349(42.17%)

Baada ya kushinda ubunge, Mbowe alipewa nafasi ya kuunda serikali Mbadala yaani Kambi Rasimi ya Upinzani Bungeni (KUB/KRUB) huku akisaidiwa na Naibu kiongozi wa kambi rasimi ya Upinzani Bungeni Zitto Zuberi Kabwe ambaye alivuliwa nyadhifa zake mwishoni mwa mwaka 2013, Mnadhimu wa kambi Rasimi ya Upinzani Bungeni Tundu Antipas Lissu nk. Mwaka 2010 mpaka mwanzoni mwa mwaka 2014 Mbowe aliunda serikali Kivuli ya Baraza la mawaziri vivuli (Shadow government) yenye mawaziri vivuli (Shadow ministers) kutoka CHADEMA pekee yake na Mwaka 2014 Mawaziri vivuli waliongezwa kutoka vyama vya NCCR MAGEUZI na CUF.

Kati ya mwaka 2010 mpaka 2014 , Chini ya uongozi wa uenyekiti wa Mbowe, Chaguzi ndogo zimefanyika za udiwani na ubunge. Majimbo ya uchaguzi mdogo wa ubunge ulifanyika katika majimbo ya Igunga, Chalinze, Arumeru Mashariki, Kalenga huku CHADEMA ikishinda jimbo moja la Arumeru Mashariki na mengine kuangukia mikononi mwa CCM

Katika kipindi hicho hicho cha uongozi wa Mbowe 2010 - 2014, CHADEMA imefanya Operation za kichama ikiwepo Vuvuvugu la Mabadiliko (Movement For Change-M4C),CHADEMA ni Msingi, Pamoja DAIMA. Operation hizo zilileta changamoto kubwa kwa siasa za CHADEMA mfano kejeli ya "COPPER TATU KATA TATU"   operation ambayo kwa kiasi kikubwa ilikua ni kudhibiti madhara zaidi ya kufukuzwa Zitto Kabwe ambaye vijana wake walifanya Kazi kubwa kuhujumu CHADEMA Kwa njia halali na za nuruni, gizani na mafichoni ikiwa ni Pamoja na kuchoma bendera za CHADEMA, kadi, kushusha bendera za CHADEMA na kupandisha za ACT Wazalendo na CCM, kutoa matamko ya kupinga CHADEMA na Viongozi, matusi na kejeli nyingi.Hata hivyo Operation hizo zimesaidia CHADEMA kushinda serikali za mitaa nchi nzima ikiwepo kusini pamoja na uchaguzi mkuu mwaka 2015 ambapo CHADEMA na  UKAWA kwa ujumla imevuna majimbo Mtwara, Lindi, Tabora, Tanga, Dar Es Salaam nk ambazo zilikuwa ngome za CCM.

Pia ni kipindi hiki, CHADEMA iliungana na vyama vingine vya CUF, NCCR, ND NA DR ingawa kilijitoa baadaye kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)  mwezi Septemba 2013 na kuuimarisha zaidi mwaka 2014 na 2015

Septemba 14, 2014,Freeman Mbowe aligombea tena Uenyekiti wa CHADEMA akipambana na Gambaranyere Mwagateka. Katika uchaguzi huo, Freeman Mbowe aliibuka mshindi kwa kupata kura 789 huku mpinzani wake Gambaranyere Mwagateka akijipatia kura 20.

Disemba 14,2014 ulifanyika uchaguzi wa Serikali za mitaa nchi nzima kasoro Sumbawanga mjini na maeneo machache. CHADEMA na UKAWA kwa ujumla ilipata ushindi katika maeneo mbalimbali nchini hata ngome za Ccm. Mfano, Wilaya ya ILEJE ambayo mwaka 2009 CHADEMA ilikua na kijiji kimoja tu Cha Ikumbilo lakini katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2014 ilivuna vijiji 22 na CUF kijiji 1 na kuifanya Ileje kuwa wilaya ya tatu kuchagua CHADEMA Mkoa wa Mbeya. Hali ilikua hivyo Dar Es Salaam, Tanga, Mwanza, Kigoma, Mtwara, Lindi nk

Katika uchaguzi Mkuu mwaka 2015,Freeman Mbowe aligombea ubunge jimbo la Hai na kushinda kata zote 16 kasoro moja ya  17 ambayo uchaguzi uliahirishwa baada ya mgombea kufariki. Mbowe alishinda uchaguzi kwa kupata kura 51,124 huku mgombea wa CCM Dastan Mally akipata kura  26,996,Nuru Muhammed wa  ACT Wazalendo akijizolea kura 315 na  Ndashuka Issa wa APPT - Maendeleo akijinyakulia kura  279.

Katika nafasi ya Urais, Mbowe na kamati kuu walishirikiana kumuingiza Edward Lowassa ndani ya  CHADEMA na kupeleka Jina Lake Baraza kuu na hatimaye kupitishwa na Mkutano mkuu wa CHADEMA tarahe 04/08/2015 kama mgombea urais wa CHADEMA anayeungwa mkono na UKAWA. Lowassa alijipatia kura zaidi ya milioni 6 kwa mujibu wa Tume ya uchaguzi chini ya Jaji Damian Lubuva huku CHADEMA ikisema imeshinda uchaguzi kwa 62% dhidi ya CCM na vyama vinginevyo.

Baada ya uchaguzi Mkuu 2015 , Freeman Aikael Mbowe aliunda Serikali mbadala (Shadow Government) au Kambi rasimi ya Upinzani Bungeni (KUB/KRUB) mapema mwaka 2016 ambayo inahusisha vyama vyote ndani ya UKAWA.....
      
              ******MWISHO******
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO