Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

NAIBU MEYA WA JIJI LA ARUSHA MH VIOLA LIKINDIKOKI NA MADIWANI WAWILI VITI MAALUMU WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI ALASIRI YA LEO

Taarifa tuliyopokea kutoka kwa Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mh Kalisti Lazaro inaeleza na kuthibitisha kuwa Naibu Meya wa Jiji la Arusha Mh Viola Lazaro Likindikoki  anashikiliwa na Jeshi la Polisi kitengo cha Cyber Crime kuanzia majira ya saa 9:20 alasiri ya leo.
Mh Viola amekamatwa Ofisini kwake (Ofisi ya Mstahiki Meya) akiwa anatekeleza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.

Wengine waliokamatwa na kushikiliwa na Jeshi hilo ni madiwai viti maalumu wote kutoka CHADEMA Mh Sabina Peter, Happiness Elia Chale ambao walikuwa pamoja nae kwenye Ofisi hiyo ya Mstahiki Meya.
Sababu za kushikiliwa kwao bado hazijajulikana wazi lakini kwa sasa wanachukuliwa maelezo kwenye kitengo cha Cyber, Polisi Mkoa wa Arusha.


Mh Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Viola Likindikoki katika moja ya maukioya kamapeni za kisiasa (Picha ya Makataba)

Mh Sabina Francis, Diwani Viti Maalumu Halmashauri ya Jiji la Arusha
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO