Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe |
Jana jioni katika kipindicha Jahazila Clouds Fm kulikuwanataarifa ya mahojiano ya moja kwa moja kutoka studio na Mmiliki wa shamba la mboga mboga Machame, Mh Mbowe na watangazaji wa kipindi akiwemo EphraimKibonde lengo likiwa ni kupata uhakika wa taarifa za Mkuu wa Wilaya ya Hai kuongoza kikosi kilichoteketeza shamba na miundombinu ya gharama kubwa.
Mtangazaji wa Jahzi la Clouds FMjana jioni, Ephraim Kibonde anamuuliza kama taarifa zinazosambaa mitandaoni ni za kweli
Mimi niko Dodoma kuendelea na vikao vya Bunge. Ni kweli nimepata taarifa ya Mkuu wetu wa Wilaya ya Hai (Gelasius Byakanwa) akiambatana na askari, askari wa mgambo na watu wengine ambao sijaweza kuwafahamu wakiwemo vilevile waandishi wa habari, walikwenda kwenye mradi wetu (familia) ambao ni wa kilimo cha kisasa cha Green House tukilima mboga na matunda kwasababu ya local market na kwa sababu ya export market, na wakaanza kudestroy miundombinu ikiwemo kuharibu green house, kukatakata mabomba, kuharibu mimea na uharibifu mwingine.
Sasa taarifa nilizozipata kutoka kwa wafanyakazi walioko site ni kwamba wanadai kuna maelekezo ya NEMC kwamba kilimo tunachokifanya kinaharibu mazingira kwa hiyo hatustahili kuendelea na kilimo kile.
Mtangazaji akauliza, waliwapa barua rasmi?
Tulipokea barua ya NEMC ya Alhamisi tarehe 7 tukaipata tarehe 8 na tuliijibu hiyo order ya NEMC na kuwaambia kwamba tunaamini wamekosea sheria kwasababu kilimo chetu hakiharibu mazingira wala shutuma zilizotolewa kuhusiana na kilimo hicho si kweli. Kwamba wanadai ushamba hilo limeanzishwa katika chanzo cha mtu Weruweru jambo ambalo sio kweli. Mto Weruweru unaanzia mlimani kabisa huko Kilimanjaro National Park na umekuwepo kwa miaka na miaka na hilo ni shamba la Kifamilia ambalo tumekuwa tunalilima kwa miongo zaidi ya mitatu kabla sijazaliwa, kabla ya nchi hii haijapata Uhuru. Tulikuwa tunalima na watu wa jirani nao wanalima lakini unashangaa jambo kama hilo linafanyika Kijijini tena nyumbani kwangu.
Mkuu wa Wilaya ameamua kujifanya ni mtekelezaji wa amri ya NEMC, amekwenda site amevunjavunja na kuharibu mali.
Ni jambo la kufedhehesha sana kwamba tunawashawishi wawekeze katika Kilimo, tena kilimo cha kisasa lakini viongozi wetu hao wa Serikali bila hata kuheshimiana wanakuja wanaharibu uwekezaji wa watanzania. Wanaharibu uzalishaji wa mazao, wanaharibu miundombinu. Sisi tumepokea hizo taarifa, ni za kusikitisha. Wametusababishia hasara kwenye mamilioni ya fedha.
Askari Mgambo wakiondoa miundombinu ya umwagiliaji katika shamba la Kilimo cha Kisasa cha Mboga mboga la Kilimanjaro Vegees Ltd linalomilikiwa na Mbunge wa Himbo la Hai,Freeman Mbowe. |
Alipoulizwa na mtangazaji Ephraim Kibonde: Mbona kama wanakuandama?.. Au na wewe ni makinikia?
Ni kwasababu ya misimamo yangu kisiasa, kwasababu ya muelekeo wangu kisiasa na udhabiti na uimara wa chama ninachokiongoza.
Na mimi siwezi kuwa kondoo. Nimesema siku zote, haya mambo ya Duniani anayeyalipa ni Mungu sio mtawala yeyote yule, wala hawatanibadilisha mawazo yangu kwa kuharibu mali zangu.
Wanaweza kuharibu zote hata wakitaka roho yangu waichukue tu lakini haitabadilisha msimamo wangu katika kuamini ninachokisimamia ninachokipigania katika Taifa.
Hakuna wingi wa mali ambao wataharibu utakaonifanya Mbowe niwapigie magoti kama wengine wanavyopiga magoti. Sitapiga magoti, nitasimama katika kweli na haki wakati wote wa maisha yangu.
Kwa hiyo, jambo hili mimi halinishangazi kwasababu najua gharama ya ninacholipa. Wako watu wengi wamenipigia simu kijaribu kunipa pole, kunitia moyo. Wengine wanajaribu kunitia hofu na kuniambia Mwenyekiti Mbowe uachane na siasa, nawaambia sitaachana na siasa. Nitafanya siasa alimradi ni siasa safi yenye kusimamia ukweli na haki, nitasimama nazo!!
Moja ya mazo katika shamba la Kilimanjaro Vegees Ltd |
0 maoni:
Post a Comment