Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

NASSARI AENDELEA NAUTEKELEZAJI WA AHADI JIMBONI - ACHANGIA SIMENTI MIFUKO 100 UJENZI WA ZAHATI YA KING'ORI

Ofisi ya Mbunge Jimbo la Arumeru Mashariki Mhe Mbunge Joshua Nassari leo imekabidhi cement mifuko 100 na mchanga katika kata ya King'ori kijiji cha Nsengony ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Mbunge kufanikisha ujenzi wa Zahanati itakayojengwa katika kijiji hicho.
Katika makabidhiano hayo Mhe.Mbunge aliwakilishwa na Diwani wa kata ya Imbasen Mhe.Gadiel Mwanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Meru aliyeongozana na Katibu ofisi ya Mbunge Julius Ayo, Diwani Kata King,ori  Mhe Peter Kesy mwenyeji na Diwani wa Kata ya Maruvango
Mhe Samwel Nnko.
Diwani wa kata hiyo Mhe Peter Kesy naye alichangia vifaa tiba kwa ajili ya zahanati hiyo inayotegemewa kuanza kutoa huduma mda wowote.
Aidha, Mhe Mbunge ametoa fedha kiasi sh million 2 kwa ajili ya furniture (Samani) za zahanati ya Kijiji cha Maruvango Kata ya maruvango iliyoibuliwa na Diwani wa Kata hiyo Mh Samwel Nnko pamoja na wadau wa maendeleo na wananchi Zahanati hiyo imekamilika tayari .


Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO