Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

PICHA ZA TUKIO LA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA HAYATI DK PHILEMON NDESAMBURO UWANJA WA MAJENGO MOSHI LEO

NDESAMBURO AACHA REKODI
Moshi Kilimanjaro. 
Mwili wa mbunge wa zamani wa Moshi Mjini kupitia Chadema (2000-2015), Philemon Ndesamburo jana uliweka rekodi ya aina yake mkoani Kilimanjaro kwa kuagwa na kuhudhuriwa na maelfu ya waombolezaji.
Haijapata kutokea tangu Uhuru wa nchi hii kwa kiongozi kuagwa uwanjani na watu wengi kwani kumbukumbu zinaonyesha wote waliomtangulia ama waliagwa nyumbani kwao au katika makanisa waliyokuwa wakisali.
Awali, Ndesamburo alikuwa aagwe katika Uwanja vya Mashujaa ili kuakisi ushujaa wake wa kuwaletea maendeleo wananchi wa Moshi, lakini Serikali ilizuia.
Hata hivyo, pamoja na kuzuia shughuli ya kufanya kumbukizi na kutoa heshima za mwisho katika uwanja huo na kuhamishia shughuli hiyo katika Uwanja wa Majengo, bado tukio hilo liliutikisa mji wa Moshi.
Mapema jeneza lililobeba mwili wake lilipangiwa kutembezwa katika mitaa na barabara mbalimbali za mji huo, lakini polisi ikazuia ikisema hayo yangekuwa ni sawa na maandamano. Hata jeshi hilo lilipoelekeza msafara huo utoke hospitali ya rufaa ya KCMC hadi Uwanja wa Majengo, bado barabarani watu walikusanyika kuuaga mwili huo hali iliyowapa wakati mgumu polisi.
Kuanzia saa 4:20 asubuhi, polisi wa kutuliza ghasia wakishirikiana na askari wa usalama barabarani, walianza kujipanga katika mzunguko wa magari wa YMCA ili msafara usiingie katikati ya mji.
Polisi hao wakiwa na magari matatu na silaha walijipanga na kuelekezana namna watakavyohakikisha msafara huo hauingii mjini kama jeshi hilo lilivyokuwa limetoa maelekezo.
Msafara ulipokaribia shule ya msingi J.K Nyerere (zamani Kibo) polisi walitumia mbinu ya kukamata magari ya kiraia na kuyatumia kuziba barabara inayoelekea mjini ili kuhakikisha hakuna gari linapita.
Kutokana na ukubwa wa msafara wa magari likiwamo lililobeba mwili wa Ndesamburo, barabara zote zinazoingia na kutoka katika mzunguko huo wa YMCA zilifungwa isipokuwa ya kuelekea Majengo.
Baadhi ya madereva waliokuwa wakienda barabara kuu ya Moshi-Dar es Salaam walilazimika kutumia barabara mbadala, ingawa hata huko mbele walikutana na vizuizi vya polisi wakiwamo wa usalama barabarani.
Msafara huo ulitanguliwa na waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda na kisha watembea kwa miguu ambao walitembea kuanzia maeneo ya madukani hadi Uwanja wa Majengo.
Mbali na pikipiki na watembea kwa miguu, msafara huo ulikuwa na magari zaidi ya 50 yaliyowabeba baadhi ya viongozi wa kitaifa ambao walilazimika kwenda mwendo sawa na wa watembea kwa miguu.
Mamia ya wananchi walijipanga katika barabara nzima kuanzia KCMC hadi Uwanja wa Majengo huku baadhi ya wananchi wakitumia simu zao za mikononi kupiga picha za kumbukumbu.
Msafara ulipofika uwanjani, ulipokewa na wabunge, madiwani na watu waliopata shahada ya udaktari wa heshima (PhD) pamoja na marehemu ambao walipata fursa ya kubeba jeneza lake.
Pia, washirika hao waliopata heshima hiyo pamoja na Ndesamburo walifanya tendo la kuweka joho na kofia ya Ndesamburo aliyotunukiwa juu ya jeneza lake.
Maelezo: MWAANCHI


Baadhi ya nukuu zahotuba za viongozi waliohutubia uwanjani hapo

Mh Fredrick Sumaye
"Kuna juhudi kubwa sana ya watu kujidanganya kwamba wanaweza kukandamiza demokrasia hii tulipofikia. Demokrasia ni kama 'ball bladder, ukiikandamiza sanaitapasuka.... Chuki sasa ipo dhahiri. Hizi chuki tukiendelea kuzijega hazitaacha mtu hai. Chadema ina watu wengi sana.Hatutaweza kuwaonea muda mrefu"

Mchungaji Peter Msigwa
"Uongozi ni kuongeza thamani kwa watu unaowaongoza, na ndicho alichokifanya Ndesamburo. Tujifunze tutakapokuwa tumekufa tutaacha nini nyumba yetu. Haitakuwa kuhusu muda gani umeishi duniani bali umesaidia nini. Viongozi wa Serikali wajiulize pale ving'ora vinapoondoka na askarihawapo, utapata mapokezi kama haya"

Mh Edward Lowassa
"Niungane na Sumaye na Gwajima. Jitihada zakudidimiza demokrasia zinaendelea kwa kasi sana. Baada kuwakatalia uwanja wa Mashujaa mmeamua kuja Majengo. Hawa tuwasamee bure!"
Mama Mwijage wa CUF
"Wale ambao walifanya Ndesamburo asiagweuwanja wa Mashujaa Mungu anajua mwenyewe. Ndesamburo amemaliza, wao hawajui watakufa namna gani. Yeye kamaliza safari yake,sisi hatujui yakwetu?"
Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo
"Nilazima tumuenzi Mzee huyu. Kumuenzi Ndesamburo ni kuenzi demokrasia. Poleni sana Kilimanjaro. Hajaondoka mtupu, ameacha legacy. Badala ya kulia mnapaswa kumtazamana kushukuru"

John Heche, Mbunge wa Tarime
"Niwaombe viongozi wote wadini na vyama tusimame. Chuki inazidi kushamiri kwenye Taifa letu. Tunapoona watu wanazuiwa kutoa rambirambi, Mzee kama huyu anapewa mizengwe, chuki inapitiliza mtu asiagwe kwenye mahali walipopendekeza. Tukemee sana mambo haya na chuki inayopandikizwa kwa niaba ya vizazivijavyo"

Mh Ester Mmasi, mwakilishi wa wabunge wa CCM
"Wabunge wa CCM tumeguswa sana na msiba huu. Tulipozungumza (Dodoma) wengine walisema tumepotezababa..., wengine wameoteza mtu aliye adimu sana. Nimetumwa nilete salamu za rambirambi kutoka kwa RaisMagufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM. Naibu Spika (Mh Tulia Ackson) alifika nyumbani kwa marehemu akiambatana na uongozi wa CCM Kilimanjaro na Waziri Maghembe. Naibu Spikaalisema katika wasifu wa marehemu, Mzee Ndesamburo alisimama... bila kujali itikadi na msiba huu utupe nafasi ya kutafakari. tarehe 31 Mei, 2017 wabunge wa CCM walifanya ibada ya kumuombea marehemu iliyoongozwa na Jenista Mhagama. Wamejipanga kuja kibunge (kuwafariji wafiwa)"

Mh Anna Komu, Mbunge Mstaafu CHADEMA
"Ndesamburo alikuwa na masimamo wa vitu vitatu; Kusimamaia dhamira kwahali na mali, Mkweli saa zote na mwenye Upendo kwa wengine. Huwezi kuongoza watu kwakuwabagua matabaka kwa kuona wengine wana maana wengine hawana. Kiongozi lazima uwapende unaowaongoza"
Mh Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa
"...Tukaenda Polisi kuomba Brass Band ya Polisi. Wakasema Mwenyekiti ongea na IGP Simon Sirro. Leo Polisi wanaogopa hata kufanya kazi kwasababu hawajui bwana mkubwa atafurahi au atakasirika.... Wengine wanaogopa mimi niseme, kuna ukandamizaji kwa Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro."

Sheikh Rajab Katimba, Jumuia ya Taasisi za Kiislamu Makao Makuu
"Ndesamburo ndiye aliyewezesha kuweka uzio makaburi ya Moshi. Tunaomba jamii ijifunze kutoka kwa Mzee huyu na ndio tutamuenzi. Kuna hatua tano za maisha ya mwanadamu; roho kuumbwa, kuzaliwa, kuishi, kufa, kuzikwa na hukumu. Tuwasamehe wabaya ambao hawatakii mema amani ta Tanzania na msiba huu usitumiwe kama mtaji wa kisiasa. Chama (CHADEMA) kihakikishe kinatunza kumbukumbu za muasisi huyu (Ndesamburo) tukiamini kuna siku haki itakuja kutamalaki katika Taifa hili."

Mh Ester Bulaya, mwakilishi Wabunge wa CHADEMA
"Wabunge wote wa CHADEMA tumeguswa sana na msiba huu. Ndesamburo ni miongoni mwa wazee walionishauri kuungana na vijana kuleta mageuzi ya kweli. Ukikaa nae huwezi kuhisi uko na mzee. Aliniambia,Ester, huko uliko hustahili njoo huku.Simama na vijana wenzako tetea Taifa lako... Mbali na utajiri wake na heshima kubwa aliwaheshimu wasio na mali na wanyonge na mpaka anakufa alikuwa anaandika cheque kusaidia familia za watoto waliokufa (wa Lucky Vincent) bilakujali walikuwa wachama gani. Tutaendelea kupigania haki za Taifa bila kujali vikwazo vilivyoko..Hatutaki kufa tukiwanyanyasa wananchi, hatutaki kufa tukitoa adhabu kwa wananchi waliotuchagua"

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi
"Baba yetu Ndesamburo, masingialioujenga Moshi, siasa alizokuwa anaziendesha Moshi ndio mafanikio ya Manispaa ya Moshi. Hakuna mtu atakayetuondoa kwenye msingi wa amani na mshikamano aliotuachia. Nawahakikishia, kwa pamoja na Mbunge, aliyoyajenga Ndesamburo tutasimama nayo mpaka ukombozi utakapotokea... Kijana unapofanya mambo bila kutumia busara unadhalilisha vijana wenzako. Tumuombe Mungu atuongezee Busara na sio Madaraka!"

Mh James Mbatia, Mwenyekiti mwenza UKAWA na Mbunge wa Vunjo NCCR Mageuzi.
"Nilimjua Ndesamburo mwaka 1991 mwezi wa sita, wakati huo ndio tumemaliza kongamano la demokrasia. Tarehe 31 Januari 2016 Ndesamburo aliniambia tuandike historia ya mageuzi nchini na atagharamia. Akakutanana Ndimara Tegambwage kwa kazi ya kuandika. Alitaka iandikwe afurahie kazi yake duniani .

Tutamuenzi Ndesamburo kwa kuita wana mageuzi wote wakutane Moshi kuandika historia ya wanamageuzi. Tanzania ni mali ya watanzania. Niwaombe CCM, misiba kama hii inaleta watu wote pamoja. Tusikubali kufarakanishwa namna hii. Hakuna uwakilishi wa CCM hapa. Kamamwenyekiti wa kituo cha demokrasia nimewawakilisha lakini nitawaambia. Tusikubali kugawanywa namna hii. Kitendo hiki ni kibaya sana."


Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO