Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mama Mghwira aapishwa tayari kwa kazi ya Ukuu wa Mkoa Kilimanjaro

Mkuu mpya wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Anna Mghwira akiingia kwenye gari yake ramsi kwa kazi baada ya kuapishwa na Rais Magufuli asubuhi ya leo.

Picha na ISSA MICHUZI
KWA MUJIBU WA MTANDO WA GAZETI LA MWANANCHI 
Dar es Salaam
Wakati Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amekula kiapo Ikulu jijini hapa leo, Jumanne Chama cha ACT- Wazalendo kimesema kitajadili utekelezaji wa majukumu yake mapya na ya uenyekiti wa chama hicho.
ACT imesema ilipokea taarifa ya uteuzi huo wakati Mghwira akiwa nje ya nchi hivyo baada ya kurejea, viongozi wa juu wa chama hicho pamoja na yeye walifanya mazungumzo kuhusu uteuzi huo.
Mghwira aliteuliwa nafasi hiyo Juni 3, mwaka huu na Rais John Magufuli kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Saidi Meck Sadick aliyeamua kuachia ngazi ili vijana waendelee kufanya kazi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Jumanne na kuthibitishwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa ACT, Ado Shaibu ni kuwa kufuatia uteuzi huo na uenyekiti na majukumu ya Mkuu wa Mkoa kamati ya uongozi wa chama itakutana kesho kwa ajili ya mazungumzo.
Pamoja na mambo mengine chama kitajadili namna ambavyo Mghwira atatekeleza wajibu wake wa uenyekiti wa chama na majukumu yake mapya.


 “Chama kinatoa wito kwa wanachama wake kuendelea na utulivu wakati wa vikao vyake vya chama vinachukua hatua stahiki kuhusu jambo hilo,”imesema taarifa hiyo.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO