Wito umetolewa kwa waongoza watalii nchini kutoa ushirikiano ,kuwapendekeza watakaoingia katika kinyang'anyiro cha kumtafuta mshindi wa Tuzo ambayo imeandaliwa kwaajili ya kumpata Balozi atakaewawakilisha waongoza utalii nchini Tanzania,Afrika ya Mashariki na Kati .
Akizungumza na blog hii Muasisi na mwenyekiti wa Tuzo hiyo Sadock Mugetta amesema kuwa tuzo inafahamika kama TANZANIA TOUR GUIDE AWARDS ambapo mwaka jana ilikuwa imegawanyika katika vipengele vya kumtafuta muongoza watalii bora wa Mlima,Safari pamoja na Wapagazi,ila mwaka huu wameongeza vipengele viwili ambavyo ni Muongoza utalii wa Utamaduni pamoja na Mpishi bora.
Sadock amesema kuwa wameamua kuwepo kwa Tuzo hiyo kutokana hali halisi iliyopo ya ugumu wa kazi wanayoifanya waongoza watalii (Mabalozi) ili mshindi atakayepatikana atawawakilisha katika mambo yao ambayo wanataka Serikali iyafahamu,pamoja na wageni mbalimbali waitambue Tanzania pamoja na vivutio vya Utalii vilivyopo.
Ameongeza kuwa tangia kuanzishwa kwa huduma ya utalii hapa nchini waongoza Watalii hawajawahi kupewa kipaumbele, hivyo ni vyema Serikali ikatambua kuwa muongozaji watalii huwa anatumumia 99% ya muda wao kukaa na mgeni awapo nchini na anapewa taarifa zote sahihi na muhimu hadi anaondoka nchini.
"Ikumbukwe kuwa tangia kuanzishwa kwa huduma hii ya utalii waongozaji hawajawahi kupewa kipaumbele wakati anatumia 99%ya muda wake na mgeni akiwa hapa nchini ,anahakikisha mgeni yupo salama,anahakikisha mgeni anapata taarifa zote sahihi hadi anaondoka nchini,muongozaji huyu anafanya kazi yake kama mwalimu,Daktari pale mgeni anapopata taizo anampatia huduma ya kwanza,mpishi,mpatanishi na Balozi mwaminifu".alisema Sadock.
Kwa upande wake Katibu wa Waongoza watalii wa kujitegemea Ally Mtemvu amesema kuwa hakuna mgeni anayekuja nchini kufanya utalii pasipokuwa na muongozaji amesema tuzo hiyo inawashirikishwa makampuni yote ya utalii ,wadau wa utalii KIATO,TATO, pamoja KGA,TTGA,FGST,KTAS,TTG,KILIMERU,TPO,MMPA,NCPG na NMPA
" Hivyo tunaiomba Wizara ya Utalii na Maliasili watuunge mkono kuhakikisha kuwa tuzo hii ya Afrika Mashariki na Kati zinakuwa bora zaidi kwakuwa tumewatangulia na imeasisiwa nchini Tanzania "alisema Ally.
Aidha Tuzo hii ilizinduliwa rasmi mwaka 2016 mkoani Arusha ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Anjelina Madete,ambapo mwaka huu 2017 itafanyika jijini Dar es salaam kwenye maonyesho ya SITE october 13-15,2017 ambapo mgeni rasmi atafahamika hapo baadae.
Mwisho wa mapendekezo ya majina ni tarehe 30/6/2017
0 maoni:
Post a Comment