Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimeitisha mkutano wa dharula wa wanasheria nchi nzima kwa ajili ya kujadili mapendekezo na kutoa msimamo wao dhidi ya Serikali ya kuanzisha Bodi ya Usajili ya Mawakili.
Akizumza jana kwenye mkutano huo Rais wa TLS, Tundu Lissu alisema mapendekezo yaliyotolewa ni hatari kwa uhuru wa TLS na kada ya sheria kwa ujumla iwapo siasa itaingia kwenye kazi zao za sheria.
Alisema bodi hiyo ikianzishwa itakuwa chini ya waziri wa sheria na katiba na ndiyo itakuwa na nguvu ya kusajili au kuwafuta wanasheria kadri itakavyoona inafaa.
"Mabadiliko haya ni hatari sana kwa uhuru wa wanasheria nchini, tumekutana hapa kuelezana na kupokea maoni ya wanachama kisha tutaweka msimamo wetu baada ya baraza la TLS kukaa .
"Huo ni mkakati wa Serikali kuminya uhuru wa TLS ili kuwadhibiti wanasheria kuingia kwenye siasa, jambo ambalo linatakiwa kupingwa na kila mtu kwa sababu matokeo yake ni mabaya"alisema Mh. Tundu Lissu.
Mbali na hayo Lissu aliwaasa wanasheria kuwa endapo watashindwa kusimamia taaluma yao vizuri na kuruhusu siasa ikaingia ndani yake basi haitokuwa na maana ya kuwepo kwa chama hicho
0 maoni:
Post a Comment