Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Mh Viola Likindikoki (watatu kutoka kulia) akiwa na viongozi wa BAWACHA Arusha pamoja na madiwani wenzake waliokuwa wamekamatwa na kushikiliwa na Polisi tangu saa tisa alasiri jana mpaka usiku wa kuamkia leo majira ya saa sita walipoachiwa kwa sharti la kuripoti tena kituo kikuu cha Polisi Arusha leo asubuhi. Viongozi hao waliripoti hiyo asubuhi leo na kuelekezwa kurudi tena siku ya Jumatano Juni 28 mwaka huu.
Taarifa ambazo blogu hii imezipata zinaeleza kuwa katika kukamatwa kwao na kupelekwa kitengo cha makosa ya mitandao, kuna simu ya Naibu Meya huyo Polisi wanaitafuta, ambapo pia na mwenye nayo nae anaitafuta kwani anadai alinyang'anywa mkoba wake uliokua na vitu vyake vyote.

Dodoso zetu zinaonesha kuna malalamiko kutoka kwa Mkurugenzi wa Jiji kwenda kwa Jeshi la Polisi kuhusiana na taarifa fulani ambazo zinadaiwa kuwa za siri na mkurugenzi kuwahisi viongozi haohuenda ndio waliovujisha.
0 maoni:
Post a Comment