Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Bi Mariam Maliwa akifatilia kwa karibu Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
Afisa Utumishi Manispaa ya Ubungo Ndg Alute Joseph akitoa ufafanuzi wa kanuni za maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma
Leo June 20, 2017 watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wameanza kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano mkubwa uliohudhuriwa na watumishi wote wa makao makuu katika ukumbi wa Manispaa hiyo mkutano ambao umeongozwa na Afisa Utumishi Mkuu wa Manispaa hiyo Ndg Ally Juma Ally kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo.
Akiongea katika kikao hicho mara baada ya kufungua kikao Afisa Utumishi mkuu aliwajulisha kuanza rasmi kwa wiki ya utumishi na kutoa utaratibu wa jinsi Halmashauri itakavyotimiza maadhimisho hayo ambapo alisema kuwa kwa wiki hii ya maadhimisho muda wa kutoka kazini utaongezeka kwa saa moja badala ya kutoka saa tisa na nusu mchana itakuwa ni saa kumi na nusu, hali kadhalika alisisitiza mambo ya kuzingatia katika wiki hii na hata baada ya maadhimisho no pamoja na Kufanya kazi kwa kuzingatia sheria,kanuni taratibu na miongozo mbalimbali ya utumishi wa umma, Kufanya kazi zetu kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, na Kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa bila ya viashiria vya kupokea rushwa au hongo katika kutoa huduma katika ofisi za serikali au umma.
Mengine ni Kuongeza Ari na kujituma katika kutekeleza majukumu yetu, Kufanya kazi kwa maarifa na kuwasikiliza wanaanchi wanapofika kupata huduma katika ofisi za umma/serikali na Kuweka vizuri kumbukumbu za wananchi watakaohudumiwa kwa kipindi hiki ili kuzitolea taarifa kwenye mamlaka husika.
Pia wamesisitizwa kutoa Huduma bora, Utii kwa serikali, Kuongeza bidii ya kazi, Kutoa huduma bila upendeleo, Kufanya kazi kwa Uadilifu, Uwajibikaji kwa Umma, Kuheshimu sheria na taratibu za kazi, na Matumizi sahihi ya Taarifa.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
0 maoni:
Post a Comment