Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MUFTI MKUU WA TANZANIA AWASILI KILIMINANJARO KWA SWALA YA EID EL FITRI KITAIFA


Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery akiwa katika lango la kutokea eneo la watu mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) alipowasili jana mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya Swala ya Idd El- Fitr inayotaraji kufanika kitaifa mkoani humo.
Mufti wa Tanzania ,Sheakh Abubakary Zubery akitia aini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kilimajaro (KIA).
Mufti Mkuu wa Tanzania ,Sheakh Abubary Zubery akiteta jambo na Sheakh Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Msafara wa Mufti ukitoka katika uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) .
Mufti wa Tanzania ,Sheakh Abubary Zubery akiwa na viongozi pamoja na waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kuwasili mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wanawake wa Dini ya Kiislamu walipofika kwa ajili ya kumpokea Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery.
Mufti wa Tanzania ,Abubakary Zubery akiwasili katika mmoja wa miskiti iliyopo wilayani Hai kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi. 
Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery akifungua kitambaa katika jiwe la Msini kuashiria kuendelea kwa ujenzi wa jingo hilo litakalo tumika kama Madrasa.
Jengo la Ofisi za BAKWATA wilaya ya Hai ambalo Mufti wa Tanzania ,Sheakh Abubakary Zubery amefika kwa ajili ya uzinduzi wake.
Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery akisalimiana na waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kuwasili katika ofisi za Bakwata wilaya ya Hai ka ajili ya ufunguzi wake.
Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery akizindua rasmi ofisi za BAKWATA wilaya ya Hai.
Mufti wa Tanzania ,Abubakary Zubery akitia saini katika kitabu cha ageni mara baada ya kufungua rasmi ofisi za BAKWATA wilaya ya Hai.
Msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai
Mufti Mkuu wa Tanzania ,Abubakar Zubery akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika mskiti wa masjid Shafi kwa ajili ya uzinduzi.
Mufti wa Tanzania ,Abubakary Zubery akizindua rasmi Msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Katibu wa Bakwata wilaya ya Hai,Mwl Mohamed Mbowe akisoma risala wakati wa uzinduzi rasmi wa msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai.
Mufti wa Tanzania ,Abubakary Zubery akizungumza mara baada ya kuzindua Msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO