DIWANI wa Kata ya Murriet mkoani Arusha kupitia Chama Cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) Credo Kifukwe ajiuzulu nafasi yake.
Kifukwe amesema kuwa ameamua kujiuzulu nafasi yake ili aweze kupata muda na nafasi ya kuitumikia wananchi na familia yake na bila kuweka itikadi mbele.
"Ninajiuzulu nafasi yangu ili niweze kumuunga mkono Rais Magufuli katika utendaji wake, dhamira inanisuta kuwa katika kundi linalopinga kila kitu mimi binafsi nipo tayari kushirikiana bega kwa bega" alisema Kifukwe.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Amani Golugwa akalizungumzia tukio hilo na kueleza kwamba
"Wanaotaka kuondoka waondoke sasa, kazi tuliyo nayo ni kubwa mbele yetu. Kamwe hatutahesabu hasara yoyote kuondoka. Kazi iliyopo mbele yetu ni kubwa na yenye kuhitaji kujitoa kwa dhati. WanaCHADEMA msisikitike, wamechelewa kuondoka na msione kuwa wanatushtukiza, hapana wao ndio wamekaa kwa mateso sana na sasa hawana budi kuondoka maana hawakuwa Wa kwetu.
Yai likishakuwa viza halina thamani tena ya kukaa kwenye trei LA mayai mazuri". Wataondoka kadhaa, tusipaniki tuwaache waondoke, tulijua baadhi yao wataondoka na tunajua baadhi yao wapo njiani kuondoka, tuwaache waondoke kwa kujichinja wenyewe.
Kazi iliyopo mbele yetu ni kubwa na inahitaji waliojitoa hasa na wenye mapenzi mema na nchi hii na sio unafiki. Hila yao kwa kupindi walicho kaa nasi na dhambi yao ya maneno ya uongo wakati wa kuondoka kwao watailipa tu"
Blogu hii ilimtafuta Mwenyekiti wa CHADEMA WIlaya ya Arusha Mjini Derick Magoma ambaye alieleza kwa kifupi kuwa ndio anaingia nchini toka safarini na hajapata taarifa rasmi ya maandishi kama taratibu zilivyo kuthibitisha kujiuzulu kwa Diwani huyo ingawa alisisitiza kuwa kulikuwa na masuala ya kindidhamu dhidi yake yalikuwa yanaendelea ndani ya chama.

0 maoni:
Post a Comment