Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

ZIARA YA RAIS MKOANI PWANI: RAIS DK. MAGUFULI AZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI RUVU JUU MLANDIZI; AZINDUA VIWANDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge, Balozi wa India hapa Nchini Sandeep Arya, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo pamoja na Viongozi wengine wa Mkoa wa Pwani na Serikali akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mradi Mkubwa wa Maji wa Ruvu Juu Mlandizi Mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge mara baada ya kuzindua rasmi Mradi wa huo wa Upanuzi wa mtambo wa kusafisha maji Ruvu juu Mlandizi Mkaoni Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Archard Mutalemwa  mara baada ya kuzindua mradi huo Mkubwa wa maji.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia hatua za usafishaji wa maji katika kituo cha kusafisha maji ya Ruvu juu Mlandizi Mkoani Pwani, kushoto ni Mtendaji mkuu wa DAWASCO Eng. Cyprian Luhemeja akitoa maelezo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma pamoja na Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada uzinduzi wa mradi huo mkubwa wa kusafisha na kuzalisha Maji kwa miji ya Pwani na Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ujumbe aliotumiwa na Waziri mkuu wa India Narendra Modi kupitia Luninga kabla ya kudua Mradi huo wa maji.
 Sehemu ya Mradi huo wa maji wa Ruvu juu Mlandizi Mkoani Pwani
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Mfuko wa sandarusi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo kabla ya kuzindua kiwanda cha Global Packing kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kiwanda cha kutengeneza  matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilijaribu Trekta mojawapo katika kiwanda cha kutengeneza  matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage kabla ya kufungua kiwanda cha Nondo cha Kilua Steel Group kilichopo Mlandizi mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akipeperusha bendera kuashiria kuiruhusu treni ta TRL kusafirisha nondo kutoka kwenye kiwanda cha Nondo cha Kilua Steel Group kilichopo Mlandizi mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   pamoja na viongozi wengine akifungua kiwanda hicho cha nondo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi kwenye sehemu ya kiwanda cha kutengeneza  matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kuzindua Mradi wa maji wa Ruvu juu Mlandizi mkoani Pwani.
PICHA NA IKULU


Na. Vero Ignatus ,Mlandizi Pwani. 

Rais Dkt John Magufuli ameendelea na ziara yake mkoani pwani ambapo leo amezindua rasmi mradi wa maji wa Ruvu juu uliopo mlandizi,ambapo amezindua viwanda vitatu mkoani hapa 

Akiwa Kibaha -Mlandizi Rais  amemtaka Mkurugenzi wa Dawasa Injinia Ernchard Mutalemwa kujiuzulu haraka kabla mambo mabaya hayajampata 

''Ninaifahamu historia yako,jiuzulu uwaachie vijana tukimbizane nao ,jina la Mutalemwa nimeanza kulisikia muda mrefu haijalishi hata kama waziri ni rafiki yako au baadhi ya mawaziri ni marafiki zako wewe jiuzulu."alisema

Katika uzinduzi huo amesema amefurahishwa sana na Dawasa na Dawasco kwa kazi kubwa wanayoifanya japokuwa kuna changamoto nyingi wanazozipitia. 

"Sasa ile dhambi ya wizara ya maji walau sasa inaanza kupungua ,ila mtu asipolipa bili hata kama ni mimi pale Ikulu wewe kata tumezowea kudekezana sana ,pamoja na nyie madeni mnayodaiwa lipeni."alisisitiza

Aidha amemtaka  Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge  kwenda kumalizia mradi wa maji uliopo Lindi.
"mkimaliza tu Bunge hamieni huko wewe pamoja na wataalamu wako wote hadi mtakapoumaliza''alisema

Viwanda vilivyozinduliwa ni pamoja na  kiwanda cha Nondo cha Kilua Steel Group kilichopo Mlandizi mkoani Pwani,kiwanda cha kutengeneza  matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.kiwanda cha kutengeneza  matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO