Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAKAMU WA RAIS AMALIZA ZIARA MUSOMA MJINI LEO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia wakazi wa Musoma mjini kwenye kiwanja cha Mukendo ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake mkoani humo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia boksi lililohifadhiwa samaki tayari kwa kusafirisha nje ya nchi wakati alipotembelea kiwanda cha Kuchakata Samaki cha Musoma.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kamwe Serikali haitagawa chakula kwa wananchi wavivu ambao hawataki kufanya kazi na kusubiri chakula kutoka Serikalini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassana ametoa kauli hiyo wakati akihutubia mamia ya wananchi wa Manispaa ya Musoma katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mukendo mjini Musoma.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa Serikali itapeleka chakula kwa wananchi ambao mazao yao yaliharibiwa kwa mvua au yalikauka kwa ukame au kwa  maafa mengine na sio kwa wananchi wanaokaa vijiweni mchana kutwa bila kufanya kazi wakisubiri neema ya chakula kutoka kwa Serikali.

Amewahimiza wananchi kote nchini kuendelea kufanya kwa bidii ikiwemo shughuli za kilimo na pindi wanapovuka wajiwekee akiba na waache tabia ya kuuza mazao yote wanayovuka ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa chakula kwenye familia zao.

Makamu wa Rais pia amewataka viongozi wa mkoa wa Mara washirikiane na wananchi katika kuwaelemisha mbinu bora za kilimo ili waweze kupata mazao mengi ikilinganishwa na hali ilivyo kwa sasa.

Kuhusu tatizo la uvuvi haramu, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameziagiza Kamati za Ulinzi na Usalama kufanya misako ya hali na mali katika kupambana na tatizo hilo ambalo limechangia kupunguza samaki katika maeneo mbalimbali nchini.

Ametoa mfano kwa mkoa wa Mara kuwa ulikuwa na viwanda Vinne vya kuchakata samaki lakini kutokana na shughuli za uvuvi haramu na wa kutumia sumu umepelekea viwanda Vitatu kukosa malighafi hiyo na kusitisha uzalishaji.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema jambo hilo ni baya kwa sababu limeikosesha Serikali mapato na kusababisha wananchi wakose ajira kutoka kwenye viwanda hivyo jitihada za makusudi lazima zifanyike katika kukomesha uvuvi haramu katika maeneo mbalimbali nchini hasa katika Ziwa Victoria.

Aidha, Makamu wa Rais ameeleza kufurahishwa na kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji wa Musoma ambao umetekelezwa na Serikali ya Tanzania na Serikali ya Ufaransa  na kusema kuwa mradi huo utaondoa tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa wilaya ya Musoma.
Amewataka wananchi wa Manispaa ya Musoma kuulinda na kuutunza mradi huo ili uweze kudumu kwa miaka mingi kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa Manispaa hiyo.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mara Dakta Charles Mlingwa amewahimiza wananchi wa mkoa wa Mara kuweka itikadi zao kando na washirikiane katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.

Makamu wa Rais katika ziara yake katika wilaya za Butiama na Musoma amekagua shamba la mbegu bora za muhogo katika eneo la Rwamkoma, Butiama na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Mutex hadi Buhare yenye urefu wa kilomita 9.9 katika Manispaa ya Musoma pamoja na kutembelea kiwanda cha kuchaka samaki cha Musoma.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO