Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

NENO LA SHUKRANI KUTOKA KWA YERICKO NYERERE

Image result for Yeriko Nyerere
Yericko Nyerere

Neno la shukrani kwa Watanzania.
Makamanda, ndugu jamaa na marafiki,
Kwa heshima zote naomba niwashukuru kwa kuwa nami katika kipindi kigumu nilichopitiana ninachoendelea kupitia hadi sasa,

Naishukuru familia yangu na naiomba radhi kwakuipitisha katika bonde hili la uvuli wa mauti, hii ndio njia tuliyopo na nilazima tufike tulipokusudia.

Kwa uzito usioelezeka, namshukuru sana wakili wangu msomi Mh Peter Kibatala na jopo zima la mawakili wenza, Nakishukuru chama changu cha Chadema chini ya Mwanasheria Mkuu ambae pia ni Rais wa TLS wakili msomi Mh Tundu Lissu,

Naishukuru serikali ya Chadema Dar chini ya Meya wa Jiji Mstahiki Isaya Mwita, Nalishukuru jopo la uongozi Chadema Kanda ya Pwani chini ya kamanda Mbusule C. Shillu, Afisa Oganizesheni na Uchaguzi Kanda ya Pwani, Naishukuru Chadema Wilaya ya Kigamboni chini Katibu wa Chama Kamanda Simon Magese, Nawashukuru madiwani wa Chadema Dar wakiongozwa na Mh Selestine Maufi Diwani wa Mjimwema Kigamboni, Diwani wa Mchikichini Ilala, Diwani viti Maalumu Kigamboni Mh Stela, Nawashukuru sana baraza la wazee Mbutu wakiongozwa na Mwenyekiti wa mtaa Mh Jamal Hassan Mfaume, mmekuwa silaha yangu na walezi imara katika kipindi chote.

Na mwisho nalishukuru jeshi la polisi na maafisa usalama wote waliotekeleza wajibu wao kwa mjibu wa sheria na miiko ya kijeshi, NINALAANI kwa nguvu zote MDUDU anayeitwa "MAAGIZO TOKA JUU", Huyu kwahakika anaichafua serikali ya rais wetu mpendwa Daktari John Joseph Pombe Magufuli kwakubaka haki za watu, tunayo sababu ya kumuomba rais wetu amshughulikie.

Nawashukuru watumishi na viongozi wa kiroho ambao kwa kila sekunde mnapaza sauti zenu mbele ya Mungu kuniombea, Lakini kubwa kuliko yote nawashukuru waandishi wa habari na wadau wote katika mitandao ya kijamii, Umoja na mshikamano mlionionyesha nawaomba usiishie kwangu tu, uendelee kwa wadau wote, mechi bado mbichi, imehamia mahakamani rasmi.

Sina neno linalojitosheleza katika shukrani hizi, zaidi ya kusema asanteni sana sana...
Niwahakikishie Mimi nipo imara kuliko nyakati zozote zile, Mimi na wenzangu hatutarudi nyuma katika kupigania mambo ya msingi katika taifa letu.

Tumedhamiria, na hili naomba niweke wazi, Azimio la Baraza Kuu Chadema la 27/5/2017 pale Dodoma lililotangazwa na Mwenyekiti was Chadema Taifa Kamanda wa Anga Mh Freeman Mbowe juu ya madai ya Katiba Mpya, Tume HURU ya Uchaguzi na mengineyo vitasimama kuwa ndio msimamo wangu na sitarudi nyuma kwa hofu ama ghiriba zozote, nitaishinda hofu kwa kuikabili USO kwa macho.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO