Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Kesi ya "Ndoto ya Lema" Yaahirishwa Mpaka Juali 6, 2017 baada ya Waendsha Mashitaka wa Serikali Kukosekana

Mahakama ya Wilaya ya Arusha chini ya Hakimu mkazi Kamugisha D.K iliahirisha jana kesi za uchochezi namba 440 na 441 zinazomkabili Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema mpaka tarehe 6 Julai mwaka huu kufuatia waendesha mashtaka wa Serikali kutopatikana mahakamani hapo.

Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema (kushoto) akiteka jambo na madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha; diwani James Lyatuu (katikati) wa Kata ya Unga Ltd na Md Ally Bananga Diwani wa Kata ya Sombetini nje ya viwanja vya mahakama mara baada ya kesi kuahirishwa. 


Mh Godbless Lema akiwa anawasili eneo la Mahakama ya Wialaya ya Arusha jana kusikiliza mashauri yake namba 440 na 441 kuhusu tuhuma za uchochezi kufuatia maneno anayodai kuyatoa kwenye mikutano ya hadhara kuwa ameoteshwa na Mungu kama Rais Magufuli asipobadilika na kuendelea kukadamiza wananchi atakufa.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO