Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Kibaha Maili moja katika viwanja vya Bondeni Mkoani Pwani katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu
Mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Koka kabla ya kuhutubia Wananchi wa Kibaha Mkoani Pwani. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mwananchi Azilongwa Buhali alipokuwa akimuelezea shida yake mara baada ya kuhutubia wananchi wa Kibaha Mkoani Pwani.
Na.Vero Ignatus Kibaha Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .John Magufuli ameanza ziara ya siku tatu leo mkoani Pwani ambapo itajumuisha uzinduzi wa viwanda mbalimbali mkoni hapo ,ambapo miradi mingine ya maendeleo ikiwemo barabara itazinduliwa.
Akizungumza katika uwanja wa Bwawani Kibaha Rais ameupongeza uongozi wa mkoa huo kwa kufanya kazi kwa ushirikiano kwa kuanzisha viwanda vipya 89 ambapo katika mkoa huo vipo viwanda takribani 300 isipokuwa wilaya za Rufiji na Kibiti na hii ni kutokana na mauaji yaliyopo ambapo amesema kwa sasa ndiyo hitimisho.
“Wawekezaji hawawezi kwenda kuwekeza katika wilaya hizo kutokana na mauaji yaliyopo,serikali ya awamu ya tano siyo ya mchezo mchezo watu wenye tabia hizo waache,kwani watanyooka,nawaomba msiwaunge mkono watu hao kwani wanarudisha maendeleo nyuma ,hakuna Imani yeyote ile ya dini inayoisema watu wauane,tuwaombee watu hao waokoke wabadilike.alisema Magufuli.
Amesema kuwa viwanda hivyo ambavyo baadhi vimeanza uzalishaji vitatoa ajira kwa vijana na watanzania kwa ujumla ,amesema Tanzania siyo nchi ya kuwa maskini hata kidogo kwani ni ya pili kwa kuwa na vivutio ,ina madini ya kila aina ,25% ya nchi hifadhi na ni 3 kwa kuwa na mifugo mingi barani Afrika
‘’Nitapambana huku nikimtanguliza Mungu,ili maisha ya Watanzania yaweze kuendeklea mbele,hatukutakiwa kuwa maskini hata kidogo,lazima watu wajiulize tunamahali gani tumekosea je? Na hayo makosa tuyafanyie nini “alihoji Rais.
Amewataka viongozi wote wa serikali kujitathimini kila mmoja kwa nafasi yake ,huku kila mmoja akijiuliza amewafanyia wananchi wa maisha ya chini kitu gani,amesema kuwa kiongozi akishindwa kujitathimini,ndani ya miezi sita asisubirie miaka miwili ila ajiondoe mwenyewe katika nafasi hiyo.
Aidha Magufuli amesema kuwa kila mwezi serikali inatenga fungu bilioni 18.77 kwaajili ya kupeleka kwenye mashule sambamba na hayo serikali imeboresha shule kwa kupeleka vyombo 1700 vya mahabara.
0 maoni:
Post a Comment