Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MKAKATI WA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA MATUMIZI BORA YA ARDHI WAKAMILISHWA


Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi(NLUP) Dkt.Stephen Nindi akizungumza kwa ufupi hatua iliyofika kabla ya kwenda kukabidhi rasimu hiyo katika vyombo vya juu
Mkurugenzi msaidizi nyanda za malisho kutoka wizara ya kilimo na Mifugo Bw. Victor Mwita(Kulia) ambaye alikuwa mwenyekiti wakati wa shughuli hiyo, akitoa mwongozo wa baadhi ya mambo.
Baadhi ya watumishi Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi(NLUP) wakiwa wanafuatilia kwa makini majadiliano hayo wakiwa mkoani Morogoro.
Mmoja wa wajumbe wa kikosi kazi hicho akichangia jambo wakati wa mjadala
Bi. Amina Ndiko kutoka Shirika la kimataifa la Oxfam nchini Tanzania akitoa neno la shukurani mara baada ya kukamilisha zoezi la kukamilisha mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi bora ya ardhi.
Mratibu wa programu ya Ardhi kutoka Shirika la Kimataifa la Care  Bi. Mary Ndaro akizungumzia mambo mbalimbali ikiwemo changamoto kubwa iliyopo inayochangia ucheleweshaji wa upimaji wa ardhi ni pamoja na kuwepo kwa bajeti ndogo
Bw. Emanuel Msofe kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Idara ya Misitu na Nyuki akichangia jambo wakati wa kukamilisha mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi bora ya ardhi
Kikosi kazi wakiendelea na kazi ya majumuisho
Bw. Zakaria Faustin Mratibu wa kitengo cha Ardhi  na uwekezaji kutoka (TNRF) akizungumza jambo wakati wa majumuisho hayo.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa kikosi kazi


Kikosi Kazi cha Masuala ya Matumizi ya Ardhi kinachojumuisha wadau kutoka serikalini na asasi za kiraia wamekutana na kukamilisha rasimu ya mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi ya ardhi nchini. Mkakati itakayowasilishwa katika ngazi ya juu endapo utatekelezwa ,kusimamiwa na kufatiliwa kwa umakini kwa asilimia kubwa nchi ya Tanzania itakuwa ni miongoni mwa nchi zenye utulivu wa migogoro ya ardhi
 
Miongoni mwa wadau hao waliohudhuria katika kikao wapo kutoka taasisi za serikali na zisizo za serikali ikiwemo  Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi(NLUP),Shirika la kimataifa la Care pamoja Shirika la Oxfam.

Akizungumza  Mkoani Morogoro ,Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi(NLUP) Dkt.Stephen Nindi alisema  endapo rasimu hiyo itapitishwa na yale yaliyokuwepo ndani ya rasimu yakasimamiwa na kufatiliwa vizuri kwa kiasi kikubwa itawezesha vijiji na Wilaya kuwa na mpango mzuri wa  matumizi bora ya Ardhi.

“Ndani ya rasimu hiyo imeweza kuchambua vizuri suala zima la matumizi ya Ardhi ambayo kwa kiasi kikubwa itaondoa na kumaliza  tatizo la migogoro ya ardhi katika maeneo mengi ya nchi, baada ya rasimu hiyo kukamilika itaweza kupelekwa katika ngazi ya juu kwa  ajili ya kupewa baraka na kuanza utekelezaji wake.” Alisema Dkt. Nindi
Alisema kuwa kikosi kazi hicho kimeweza kutengeneza mipango ya ardhi takribani 100 kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu kikosi kazi hicho kipipo undwa.

"Ile kazi ambayo tuliifanya kipindi kirefu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka Serikali na taasisi zisizo za  kiserikali  tangu mwaka jana kwa sasa imefikia katika hatua ya mwisho ya  kuwasilishwa katika vyombo vya juu kwa lengo la  kupewa baraka ili utekelezaji wa jambo hilo
liweze kuanza ,"alisema Dkt Nindi

Nae Mratibu wa programu ya Ardhi kutoka Shirika la Kimataifa la Care  Bi. Mary Ndaro alisema kuwa lengo kubwa la wao kukutana na wadau mbalimbali wa mipango ya matumizi bora ya ardhi ni pamoja na kuhakikisha kuwa kuna kasi ya upangaji wa ardhi katika nchi.

"Moja ya changamoto kubwa iliyopo inayochangia ucheleweshaji wa upimaji wa ardhi ni pamoja na kuwepo kwa bajeti ndogo.Maeneo mengi yakipimwa yanasaidia kuwepo kwa usalama wa miliki na hati miliki hususani kwa wananchi wa vijijini  ambapo karibia asilimia 60 ya wananchi wanategemea ardhi kwa ajili ya kujipatia kipato hivyo kama nchi ni vema kuwekeza katika upangaji wa matumizi ya ardhi ili kusaidia kupunguza migogoro ya ardhi,”alisema Ndaro
 

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO