Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Mh Kalisti Bukhay Lazaro |
MKUU wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ametakiwa kujitathimini iwapo anastahili kuendelea kuwa mtumishi wa umma katika nafasi aliyonayo baada ya kutiwa hatiani na mahakama kuu mkoa wa Tanga na kutakiwa kulipa kiasi cha shilingi milioni 20 kwa kosa la kumdhalilisha mtumishi mwenzake kwa matusi.
Kesi hiyo namba 4 ya mwaka 2015,Gambo alikata rufaa mahakama kuu ,kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama za chini,katika kesi ya madai iliyofunguliwa na mlalamikaji ,Najum Tekka ambaye ni mwanasheria wa halmashauri wilaya ya Korogwe aliyekuwa akimlalamikia Gambo kumtolea lugha ya kumdhalilisha kuwa anadigrii ya nguo ya ndani(chupi).
Kwa mujibu wa hukumu hiyo nakala tunayo, iliyotolewa, Septemba 9 mwaka 2016 na jaji Amour Khamis wa mahakama kuu,mkoani humo,meya wa jiji la Arusha, Kalisti Lazaro alisema kuwa Gambo amekaidi kulipa kiasi hicho cha fedha kilichoamuriwa na mahakama.
Aidha meya alitoa siku saba kwa kumtaka gambo kuomba radhi kwa wanawake wote Tanzania kwa kosa la kumdhalilisha mwenzao na kwamba kinyume na hapo atahamasisha wanawake wote Arusha waandamane kupinga kitendo hicho .
Akizungumzia mwenendo wa utendaji wa Gambo katika mkoa wa Arusha,Meya wa jiji la Arusha jana, Mh Kalist Lazaro alimshauri kiongozi huyo kuangalia uwezekano wa kujiweka pembeni na madaraka aliyonayo kwa kukosa sifa na kimaadili ya kiutumishi baada ya kuwepo kwa msuguano usiokoma na baadhi ya watumishi wenzake.
Aidha alisema tangu kutolewa kwa hukumu hiyo ,Gambo amekuwa msiri na amemficha rais John Magufuli kumweleza ukweli wa mwenendo wa kesi hiyo hadi alipoteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha,jambo ambalo ni kimyume cha kanuni za utumishi wa umma.
Meya amemtaka kutekeleza mambo matano ikiwa ni pamoja na kulipa fidia na gharama zote zilizoamuriwa na mahakama ,aombe radhi kwa mwanamke aliyemkashifu kuwa anadigrii ya chupi,pia awaombe radhi wanawake wote Tanzania.
Pia alimtaka atafakari upya kiapo chake mbele ya rais kama bado anastahili kuwa kiongozi wa umma hasa ukizingatia kuwa alimficha rais kwa kiapo alichoapa wakati anafahamu wazi kuwa alishahukumiwa kwa kosa la uadilifu.
‘’Iwapo kama Gambo hata tekeleza mambo yote matano niliyotaka ayafanye ,nimejipanga mimi na wanasheria wangu tutamfikisha mahakamani kuiomba mahakama ikamate mali zake ambazo tunazijuia ikiwemo nyumba yake iliyopo Muriet jijini Arusha’’alisema meya Lazaro.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh Mrisho Mashaka Gambo |
Naye wakili George Magoti aliyekuwa akimtetea mlalamikaji katika kesi hiyo,alisema kuwa anajipanga kukaza hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo kwani licha ya mahakama hiyo kumtia hatiani kwa kumtaka kulipa kiasi hicho cha fedha ,hadi hivi sasa hajatekeleza amri hiyo.
Alisema kuwa mahakama ilimwamuru kulipa kiasi cha shilingi milioni 20 kama fidia kwa mlalamikaji,shilingi milioni 5 gharama za uendeshaji wa kesi na asilimia 7 ya riba tangu kuanza kwa kesi mwaka 2015 na kwamba kiasi hicho cha fedha kitaongezeka kutokana na muda ulioamuriwa kupita.
0 maoni:
Post a Comment