Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ANNA MGHWIRA ,ASHUHUDIA MAGARI 103 YAKIWA NA SHEHENA YA MAHINDI NJIA PANDA YA HIMO


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akiwa ameongozana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro wakiwemo Kamanda wa Polisi ,Hamis Issah na Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba wakitembelea maeneo ambayo yameshikiliwa magari yaliyobeba shehena ya Mahindi .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizunbgumza na baadhi ya wafanyabaishara wa Mahindi ambao magari yao yanashikiliwa eneo la Njia Panda mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya Wafanyabiashara ambao Mahindi yao yanashikiliwa katika eneo la Njia Panda mkoani Kilimanjaro wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira alipofika eneo hilo kwa lengo la kuzungumza nao.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiangalia magari yaliyobeba shehena ya Mahindi yanayoshikiliwa katika eneo la Njia Panda ya Himo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizungumza na baadhi ya madereva na Wafanyabaisahara ambao Mahindi yao yanashikiliwa eneo la Njia Panda ya Himo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akitizama Malori yenye Shehena ya Mahindi yakiwa yamehifadhiwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo nyuma ya vituo vya Mafuta .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiongozana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issa wakiodoka katika eneo hilo baada ya kuangalia malori yanayoshikiliwa yakiwa na shehena ya Mahindi.
Baadhi ya Magari yakiwa yameegeshwa katika maeneo tofauti tofauti yakiwa na shehena ya Mahindi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.


ENEO la njia Panda linalounganisha barabara za Moshi/Arusha,Tanga/Dar es Salaam na ile ya Holili mpakani mwa nchi jirani ya Kenya linatajwa kama kituo kikuu cha Malori yanayosafirisha Nafaka kwenda nchi jirani ya Kenya.
Uchunguzi uliofanywa na Globu ya Jamii umebaini kuwepo kwa maeneo yasiyo rasmi ya kuegesha Malori hayo ,mengine yakiwa na Matela yake ,ambako shughuli za kupakua mahindi na kupakia katika Magari Madogo aina ya fuso zinazotoka nchi jirani ya Kenya hufanyika.
Maeneo mengine yanayotajwa kuwepo na Magulio  ya Mahindi ni katika sehemu za maegesho ya magari  zilizopo katika  vituo mbalimbali vya kuuza Mafuta ,pamoja na baadhi ya nyumba za wageni ambazo zimegeuzwa Maghala ya kuhifadhia Mahindi.
Magari zaidi ya 103 yanashikiiwa katika maeneo ya Njia Panda na Himo yakiwa yamebeba Shehena ya Mahindi tayari kusafirishwa huku baadhi ya madereva wakiyatelekeza Malori yao kwa siku ya tano sasa na kwenda kusiko julikana .
Hatua iliwasukuma Wafanyabiashara wa Mahindi pamoja na Madereva kufika ofisi za Mkuu wa mkoa kuwasilisha malalamiko yao juu ya kukamatwa kwa Malori hayo yakiwa Njia Panda badala ya mpakani kama alivyo agiza Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa.
Wakizungumza nje ya jingo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Wafanyabiashara hao ,Laurance Kanyota,Nuru Madai na Mariam Ramadhan walisema wameshangazwa na hatua ya jeshi la Polisi kushikilia magari yao yalikuwa na Mahindi yakisafirishwa kuelekea mikoa ya Arusha na Moshi.
“Magari yetu yapo pale Sheli Maount Meru,yalitokea Tunduma kwenda Arusha,yalipofika pale siku ya Jumamosi madereva walienda kula siku kuu ya Idd,jana (Juzi) asubuhi  Matandiboi wakapiga simu kwamba tumezungukwa na Polisi ,tukaenda pale tukaonana na OCD tukaliza kwanini mnatushikia magari ambayo yako Njia Panda yanayoenda Arusha au Moshi ,wakajibu tumetumwa kushika magari yote ya Mahindi.”alisema Mfanyabiashara Mariam.
Alisema alimuelewa Waziri Mkuu katika agizo lake kwamba magari yaliyopo mpakani ndio yashikiliwe  na si kama lilivyofanya jeshi la Polisi kukamata magari yaliyokuwa Njia Panda kuelekea Moshi na Arusha huku wakimuomba Waziri Mkuu kutoa ufafanuzi  kwa wasaidizi wake juu ya agizo lake.
Mfanyabiashara Kanyota alisema amekuwa akifanya biashara ya kusafirisha mazao kwa njia halali ikiwa ni pamoja na ulipaji wa kodi lakini anashangazwa na hatua ya kuzuiliwa kwa  Mahindi yake ambayo amekuwa akinunua na kuyauza katika viwanda vya kutengeneza unga kwa ajili ya Chakula.
“Tulikua tunaomba Mkuu wa mkoa ajue kwamba sisi ni wafanyabiashara tunaolipa kodi halali ya serikali atusaidie tufikishe mazao yetu sehemu yanapotakiwa kufika ,Mahindi yangu yanatoka Mbeya ,mkulima aiyeniletea mimi kama Dalali ametoka Tunduma.”alisema Kanyota.
Kauli ya Serikali ya mkoa wa Kilimanjaro.
Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Kilimanjaro imepigiria msumari katika Agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la kutaifisha Mahindi pamoja na gari litakalokutwa kuanzia June 26 mwka huu likiwa limebeba na kusafirisha Mahindi kwenda nje  ya nchi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro Anna Mghwira  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa alisema jana ofisini kwake mbele ya waandishi wa habari kuwa magari 103 yaliyokamatwa Himo na Njia Panda yatahesabiwa kama sehemu ya uhujumu uchumi na kwamba yatataifishwa .
“Magari yaliyokamatwa kule Siha ,tayari tulikwisha amua kwamba yatapelekwa Nationa Milling(Ghala la chakula la taifa)  Arusha ,lakini haya ya Himo ,Waziri Mkuu Alisha agiza kwamba kuanzia tarehe 26 ,magari yote yatakayokamatwa ,Bidhaa pamoja na magari yenyewe yatahesabiwa kuwa ni sehemu ya uhujumu Uchumi ,kwa hiyo yatataifishwa.”alisema Mghwira.
Mghwira alisema baada ya mfululizo wa vikao vya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro juu swala zima la uuzaji na usafirishaji wa chakula nje ya nchi,kamati imefanyia kazi tamko la Waziri Mkuu kutaka kujiridhisha vya kutosha juu ya hali ya chakula iliyopo Kilimanjaro na mikoa ya jirani.
“Uogozi wa mkoa wa Kilimanjaro unapenda kuwatangazia wananchi wote,hususani Wafanyabiashara wa Sukari na Nafaka za Mpunga,Mchele ,Mahindi na Unga wa Mahindi ya kuwa ni marufuku kwa mfanyabiashara yoyote au mwananchi yoyote kusafirisha bidhaa hizo kwenda nje ya nchi bila kibali cha serikali”alisema Mkuu huyo wa Mkoa .
Alisema kukiuka agizo hilo ni kuhujumu uchumi wa nchi  kama ilivyo ainishwa kwenye kifungu cha 3 cha jedwali la kwanza la sheria ya uhujumu Uchumi sura ya 200 ya sheria za Tanzania na pia ni kukiuka agizo la Waziri Mkuu,kupitia waraka wake alioutoa  Mei 30,2017,uliozuia utokaji  wa vyakula na sukari kwenda nchi jirani .
Alisema kwa kukiuka sheria hiyo kunaweza kusababisha upungufu wa chakula kwenye baadhi ya maeneo nchini na kusababisha Mamlaka ya Mapato hapa nchini (TRA)  kukosa takwimu muhimu wa bidhaa zinazosafirishwa nje
“Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro imejiridhisha kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakisafirisha sukari  na nafaka hizo nyakati za usiku na hiki ndicho kinaleteleza kukosa takwimu muhimu kwa kupitia njia ambazo si rasmi kwa kushirikiana na baadhi ya askari polisi ambao sio waaminifu.
Wakati wa baraza la Idd lilifanyika kitaifa katika msikiti wa Riadha mjini Moshi,Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa alitangaza kupiga marufuku usafirishaji wa Mahindi kwenda nchi jirani na kwamba atakaye kiuka utaratibu huo atahukuliwa hatua kali za kisheria.
Mwisho.


Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO