Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Diwani James Lyatuu wa Kata ya Unga Ltd Arusha Azindua Maktaba ya Shule ya Msingi Saley Iliyofadhiliwa na Goodall FoundationSiku ya Jumatano Juni 21 mwaka huu katika Kata ya Unga Ltd ulifanyika uzinduzi wa Maktaba ya wanafunzi kujisomea katika Shule ya Msingi Saley.  Makataba hiyo itakayotumiwa na wanafunzi ngazi zote kuanzia shule ya Msingi mpaka Sekondari imetokana na ufadhili wa  Shirika la Goodall Foundation wakishirikiana na Challenge Aid International. Shule ya Msingi Unga Ltd na Saley ndiyo watakuwa wanufaikaji wakuu pamoja na wanafunzi wa baadhi ya shule jirani shule jirani.

Diwani wa Kata ya Unga Ltd Mh James Lyatuu ( mwenye suti nyeusi kulia) ameyashukuru mashirika hayo kwa msaada huo mkubwa ambo amedai utasaidia kuingua kiwango cha ufaulu katika Kata yake, na kuwaomba wasisite kuendelea kusaidia zaidi pale ambapo Mungu atawawezesha na kwamba Makataba hii itatunzwa vizuri ili kuweza kuleta tija iliyokusudiwa.
Wafadhili na baadhi ya wananfunzi wakiwa ndani ya Makataba hiyo mpya katika Shule ya Msingi Saley


Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO