Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WAUAJI KIBITI WATUMA UJUMBE KUENDELEA NA MAUAJI

tmp_20228-IMG_20170624_074323894294138.jpgSiku mbili tangu kuuawa kwa polisi wawili wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambao walikuwa kazini katika kijiji cha Bungu B, hali ya wasiwasi imezidi baada ya wauaji hao kusambaza ujumbe unaoeleza kuwa wanaendelea kusaka askari kwa kuwa ni wadhulumaji. Watu hao wametuma ujumbe mfupi ulioandika kwenye karatasi na kisha kuutuma katika mitandao ya kijamii, ukidai kuwa waliouawa (japo hawajatajwa majina yao) wanadhulumu watu kwa kutumia kazi yao. 

"Tunawatangazia wananchi tumewaua hawa kwa sababu wanadhulumu watu kwa kutumia kazi zao na yeyote atakayefanya kazi hapa au nje ya hapa tutamtafuta hadi nyumbani kwake. Sisi tumejitolea kufa kuliko kuishi, kwa hiyo dereva au raia popote uwaonapo toa taarifa iwe nyumbani au kazini", unasema ujumbe huo. "Hakuna njia ya kumaliza dhuluma isipokuwa chuma tu, hapa chuma tuuu!" 

Ujumbe huo ambao umeandikwa kwa mkono kwa kutumia kalamu ya rangi ya bluu unadaiwa kuwa unazungumzia vifo vya askari polisi wawili wa kituo cha polisi Kibiti, Sajent Salum na PC Masola waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa kazini. Mmoja wa madiwani katika Halmashauri ya wilaya ya Kibiti) jina tunalo) alisema ujumbe huo unawalenga askari wa kawaida na wa kikosi cha usalama barabarani. Diwani huyo alisema kundi hilo linalofanya mauaji katika wilaya za Kibiti na Rufiji bado lina nguvu. 

"Linaonyesha bado lina uwezo mkubwa wa kufanya mauaji na kutokomea kusikojulikana", alisema Alisema kwa sasa Serikali inapaswa kuongeza nguvu zaidi ya wapelelezi ili kukomesha kikundi hicho ambacho hakijulikani kinafanya hivyo kwa sababu zipi na wala kinakojificha. Akizungumza ujumbe huo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga alisema jeshi la polisi litaendelea kuwasaka. "Tutapambana nao tu", alisema Kamanda Lyanga na kukata simu 

Chanzo: Mwananchi
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO