Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, wamemsifu Rais Dk John Magufuli kwa maamuzi yake ya kuwachukulia hatua wale wote waliohusika katika kuiangamiza nchi na kuingia katika mikataba tata

Picha ya Maktaba: Dwani wa Kata ya Kimandolu, Rayson Ngowi (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Tindigani, Mh Moses

Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, wamemsifu Rais Dk John Magufuli kwa maamuzi yake ya kuwachukulia hatua wale wote waliohusika katika kuiangamiza nchi na kuingia katika mikataba tata, iliyoingizia nchi hasara kubwa katika sekta ya madini.

Baraza la Madiwani la Jiji la Arusha linaloongozwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na madiwani hao, walisema kuwa iwapo Rais Dk Magufuli atakwenda kwa kasi hiyo ya kufanya vema katika uongozi wake kwa kuwachukulia hatua viongozi wanzake, walioiharibu nchi na kuingia mikataba mibovu, uwezekano wa upinzani kuwepo na kufanya vema mwaka 2020, utakuwa mgumu na wapinzani watakosa hoja.

Diwani wa Kata ya Kimandolu, Rayson Ngowi amesema kuwa Rais Magufuli amethubutu na amechukua maamuzi, ambayo yamewagusa wananchi na kuona ni jinsi gani nchi ilivyokuwa ikiliwa na wajanja wachache.

Ngowi amesema hatua aliyochukua ni sawa na kiongozi wa upinzania, kwani hilo na mengine mengi ambayo anachukua hatua kwa sasa ndio wapinzani walikuwa wakipiga kelele kila kukicha, lakini viongozi wakuu wa nchi waliopita, walikuwa hawachukui hatua hivyo anapaswa kupongezwa na kuungwa mkono kwa asilimia mia.

Ukiachilia mbali siasa, Diwani Ngowi ambaye ni mchungaji wa madhehebu ya kilokole, ametoa ombi kwa Rais kufumua mikataba yote ya madini na gesi, kwani baadhi ya viongozi waliopita, walifanya hivyo kwa maslahi yao na sio ya Watanzania.

Diwani Amani Riwad wa Kata ya Engutoto jijini Arusha, alimsifu Rais kwa hatua anazochukua na kumtaka kuchukua hatua zadi kwa wale wengine, walioingizia nchi hasara kwa kuingia mikataba mibovu ambayo imetoa mwanya kwa wawekezaji kuiba rasilimali za nchi.

Amesema na kumshauri Rais kutaifisha fedha na mali zote walizochuma, wale wote walioingizia nchi hasara ili iwe fundisho kwa wengine kuwa ili wawe waoga na mali za umma.

Diwani wa Chadema Kata ya Ngarenaro, Isaya Doita amesema alichofanya Rais kwa kutekeleza ripoti mbili za madini ni jambo jema, na ni mawazo mazuri, yanapaswa kupongezwa bila ya kificho.

Doita amesema iwapo suala hilo, litakuwa na umaliziaji mzuri, nchi hii itakuwa na kiongozi na jabari na shupavu, aliyekosekana miaka mingi na anastahili kupongezwa kwa namna yoyote ile.

Chanzo: Redio5 Arusha
Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO