| ||||||
|
Picha ya pamoja
ya wadau wa Warsha ya wadau
wa Jali Ardhi.Picha na Carey Marks
Chuo
kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha kwa
kusirikiana na Shirika la maendeleo kutoka nchini Uingereza
(DfID) wameandaa warsha ikiwa na lengo la kujadili matukio ya
kitafiti ya sababu za mmomonyoko wa ardhi
uliochangiwa na matukio yaliyowahi kutokea hapo zamani,sasa na
changamoto zijazo katika wilaya ya Monduli.
Akizungumza
katika ufunguzi wa warsha hiyo mkuu wa wilaya ya monduli Idd Kimanta
ambaye alimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha amesema kuwa sababu kubwa
ambazo zinasababisha mmomonyoko wa ardhi ni pamoja na mifugo mingi zaidi
ya maeneo ya malisho,kilimo
cha mfululizo,kilimo katika maeneo yanayomomonyoka kwa urahisi ,ukataji
wa misitu,tabia za jamii zinazohama,mifumo ya umiliki ardhi ,kuongezeka
kwa kubwa idadi ya watu ,mabadiliko ya tabia nchi na mahitakji ya
nishati
.
Aidha
amesema kuwa zipo hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa katika kuzuia mmomonyoko wa
ardhi kwa kuhifadhi uoto wa asili,kupunguza kasi ya maji kwa kuweka
matuta,kutandaza majani katika ardhi haswa kwa kuotesha mimea jamii ya
mikunde pamoja na kuhifadhi uoto wa asili.
Akizungumzia utafiti huo Profesa wa Sayansi za kilimo kutoka Taasisiya Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha,Patrick Ndakidemi amesema kuwa utafiti huo ulianza rasmi novemba 2016 ukiwa na lengo la kupata majibu ya kitaalamu yanayosababisha mmomonyoko wa ardhi ambapo utafiti huo unatarajiwa kukamilika julai 2017
Nae mtafiti kutoka Chuo cha
Sayansi cha Nelson Mandela Dkt.Kelvin Mtei amesema
kuwa katika wilaya ya monduli mmomonyoko husababishwa na maji kutiririka juu ya ardhi
na huchukua virutubisho
kwenye udongo ,kukoseka na kwa uoto,mafuriko pale maji yanaposhindwa kupenya
kwenye udongo nakusababisha uharibifu.
Dkt.Kelvin amesema kuwa mmomonyoko wa ardhi umeanza kuongezeka miaka 20 iliyopita,ambapo maporomoko yameongezeka zaidi miaka 10 iliyopita, mmomonyoko huo unapeleka tope ziwani ambapo amesema utafiti huo walianza kwa kupima upenyaji wa maji kwenye ardhi,kulinganisha umomonyokaji,kupima kiasi cha mmomonyoko,upimaji kupitia picha za setilaiti na wakafanya uchunguzi wa tope kwenye mahabara . Sambamba na hayo baadhi ya washiriki wa warsha hiyo ambao hawakutaka kutaja majina yao wameiomba serikali ipitishe sheria itakayombana mfugaji asiwe na zaidi ya ng'ombe watano ambao ataweza kuwakuwahudumia na mfugaji huyo ataweza kutunza mazingira yake mwenyewe. Warsha hiyo ya siku mbili imewashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo watendaji wa vijiji vya Lendakenya ,Arkatan,watafiti kutoka chuo cha utafiti cha Seliani Arusha,Washiriki wa mashirika yasiyo ya kiserikali,ECHO,UJAMAA,TANAPA na MVIWATA,Wakulima na wafugaji kutokaa Monduli,Watafiti kutoka vyuo vikuu vya Plymouth,Exeter,na Schumacker ;Uingereza,Taasisi ya Sayansi na Tekinolojia ya Nelson Mandela. |
0 maoni:
Post a Comment