Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Ndg Amani Golugwa akipeana mkono na Mwenyekiti wa Kamati iliyoratibu hafla ya kuwakutanisha marafiki wa Chadema Arusha na nje ya Mkoa huo katika Hoteli ya Kitalii ya Snow Crest ya Jijini Arusha jana, kama ishara ya kushukuru kupokea vifaa mbalimbali vya muziki na matangazo ambavyo vitatumika kwa shughuli za chama katika kueneza vuguvugu la mabadiliko (M4C) kama linavyohubiriwa na chama hicho.
Kwa maelezo ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mh Godbless Lema, vifaa hivyo ni seti kamili pamoja na jenerator kubwa vinathamani ya zaidi ya Shilingi za Kitanzania Milioni 14, pesa ambazo zilitoka kwa marafiki hao na baadhi ya viongozi wa chama.
Akishukuru kupatikana kwa vifaa hivyo, Golugwa aliwasifu marafiki hao kwa moyo wa kujitolea kwa lengo la kusaidia nchi yao, na yeye kuahidi kutoa Sh milioni moja kusaidia upatikanaji wa gari aina ya FUSO kwa ajili ya kubebea vifaa hivyo.
Chadema Arusha kupitia Kamati maalulu waliangaa mjumuiko huo wa marafiki na kuupa jina la “M4C Join The Chain” ukimaanisha kuwataka wananchi wote wanaokerwa na hali halisi ya mambo ilivyo wajiunge na harakati za Chadema kisiasa ama kwa kushiriki kugombea nafasi za uongozi au kusaidia harakati hizo kwa namna watakavyoweza.
Mjumuiko huo uliwakutanisha marafiki mbalimbali wa ndani ya Arusha na nje ya Mkoa wakiwemo baadhi ya wafanya biashara wakubwa Jijini hapa. Chadema Makao makuu waliwakilishwa na Mwenyekiti wa Chadema Kanda Maalumu ya dar es Salaam, Henry Kileo, huku viongozi wengi wa Chadema Arusha na madiwani wote wakihudhuria, smbamba na Mh Lema na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari.
Awali kulikuwa na hotuba za kutia hamasa kutoka kwa wazungumzaji mbalimbali walioandaliwa, aliwemo dada yake na Hussein Bashe, Kauthar Mohamed Bashe aliyewapa ujasiri wanawake kushiriki nafasi za uongozi kisiasa na kuwa sehemu ya maamuzi katika jamii bila kuwaachia wanaume pekee.
Wazungumzaji wengine walikuwa ni pamoja na mwanadada aliyejitambulisha kama Aminata kutoka Korogwe Tanga ambako ana nia ya kuwania Jimbo la Korogwe katika uchaguzi mkuu ujao, pamoja na Emma Mroso aliyezungumzia tatizo la hofu miongoni mwa watanzania.
Amani alisema Chadema kwa sasa inahitaji kwenda kwa watu na kuwaonesha kuwa wana dhamira ya dhati ya kupigania maslahi ya Tanzania na watu wake na kuahidi kuwa watathakikisha wanasimamia Halmashauri zote wanazoziongoza ili ziwe za mfano kwa vyama vingine kwa misingi ya ufanisi katika kutumikia jamii.
Katika hitimisho lake Katibu huyo alitoa taarifa ya kusudio la chama chake kuwa na Wiki ya Chadema itakayofikia kilele siku ya Januari 23, 2013 siku ambayo Chadema itatimiza miaka 20 tangu kupatiwa usajili wa kudumu kama chama cha siasa nchini.
Mh Godbless Lema, mjumbe wa Kamati Kuu Chadema akifafanua jambo katika hafla hiyo. Pamoja na mambo mengine, Lema alijikita zaidi kuelezea namna harakati za chama chake zinavyokutana na vikwazo vingi kiasi cha kulazimisha kufikiria namna ya kujitegemea.
Akizungumzia upatikanani wa vifaa hivyo binafsi, Lema alisema kukodisha vifaa ni gaharama kubwa sana kiasi cha sh laki nne kwa kila mkutano na kudai kuwa chama hakina uwezo huo na hivyo njia mbadla na nafuu ni kuwa na vifaa vyao wenyewe. yeye na marafiki zake binafsi aliodai atawatafuta aliahidi kuchangia milioni 5 katika uchangishaji mwingine kwa ajili ya kupata gari la matangazo yao ambalo watalitumia kuzunguka maeneo tofauti ya nchi.
Lema laikumbushia vikwamishi walivyowahi kukutana navyo katika utaratibu wa awali wa wananchi kuchagia chama chake kwa kutumia namba 15710 ambapo alieleza kuwako kwa shinikizo toka Serikalini kwa makampuni ya simu kuwa katika makusanyo yote Chadema wapewe aslimilia 20 tu.
Mh Nassari na Lema wakishuhudia vifaa mbali mbali vya muziki vikitolewa kwenye maboksi yake yaliyotumika kuvisafirishia
Marafiki wakiendelea kutoa ahadi za michango zaidi kusaidia upatikanaji wa gari ya matangazo
Godbless Lema akiwa katika picha ya pamoja na wanakamati walioandaa hafla hiyo
Diwani wa Kata ya Levolosi na Mwenyekiti wa VIjana (BAVICHA) Mkoa, Mh Ephata Nanyaro akitangaza ahadi yake ya sh milioni moja kusaidia upatikanaji wa gari
Diwani wa Chadema Kata ya Olturato, Arumeru Magharibi, Mh Gibson aliahidi sh mil 1 na kutoa laki tano hapo hapo
Katibu wa Kamati iliyoratibu hafla hiyo, Chris Mbajo akifafanua jambo hiyo jana jioni
Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha Mjini akitambulisha wahudhuriaji kabla ya kuanza kwa shughulia yenyewe
Mh Joshua Nassari akizungumza katika hafla hiyo na kukumbushia kuwa ushindi wake ulitokana na sapoti ya wananchi na hivyo kuwasihi kuwa na moyo wa kujitolea kusaidia harakati za chama kwa nia njema
Vinywaji na usikivu kwa hotuba mbalimbali
Aminata mwenye ni ya kugombea Ubunge Korogwe
Bidhaa mbali mbali zilizokuwa zinauzwa katika hafla hiyo. Kofia, miamvuli, opener, mipira, skafu, vitambaa, bendera za magari, suti za kombati, key holder, mitandio, mabegi na bidhaa nyingine nyingi zenye nembo ya M4C
0 maoni:
Post a Comment