Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Watoto 6,838 waliomaliza darasa la saba Mkoani Arusha wakosa nafasi za kujiunga sekondari

PICHANI: WANAFUNZI WA DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI MWERE MANISPAA YA MOROGORO WAKIFANYA MTIHANI WA TAIFA WA SOMO LA HISABATI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MWAKA HUU.

Na Mussa Juma, Arusha 

JUMLA ya wanafunzi 6,838 waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka huu, mkoani Arusha, wamekosa nafasi ya kujiunga na masomo ya Sekondari kutokana na uhaba wa nyumba vya madarasa 172 .

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Evelyine Itanisa alitoa taarifa hiyo, juzi katika kikao cha kamati ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2013 mkoani Arusha.

Itanisa alisema wanafunzi hao, wanatoka  katika halmashauri sita za mkoa Arusha na ni halmashauri moja tu ya Karatu ambayo imeweza kuwachukua wanafunzi wote waliofaulu mwaka huu.

Alisema  katika jiji la Arusha  wanafunzi 2420 wamekosa nafasi kutokana na uhaba wa vyumba  vya madarasa 61, Ngorongoro wanafunzi 441 wamekosa nafasi kutokana na uhaba wa vyumba 11.

Alisema   Halmashauri ya Arusha vijijini  wanafunzi 1880 wameshindwa kujiunga na sekondari kutokana na  uhaba wa vyumba 47.

“Pia Halmashauri ya Longido kuna wanafunzi 140 ambao wanahitaji madarasa manne, Meru wanafunzi 1,159 wakiwa na mahitaji ya vyumba 29, wilaya ya Monduli wanafunzi 807 wamekosa nafasi kutokana na kukosekana madarasa 20”alisema Itanisa.

Alisema kutokana na hali hiyo, ameziagiza halmashauri hizo sita za mkoa wa Arusha kuiga mfano wa halmashauri ya Karatu, kwa kuhakikisha zinajenga vyumba vya madarasa vya kutosha  ili kuhakikisha wanafuzi wote waliofaulu wanapata nafasi.

“Ili kuhakikisha watoto waliofaulu wote wanaendelea na sekondari, kila halmashauri inapaswa ihakikishe inakamilisha ujenzi wa madarasa kabla ya februari  mwakani “alisema Itanisa.

Hata hivyo, Katibu Tawala huyo alisema kiwango cha ufaulu kwa Mkoa wa Arusha, kimekuwa kikipanda kwa miaka mitatu sasa mfululizo ambapo mwaka huu jumla ya wanafunzi 26,464 wamefaulu mitihani kati ya wanafunzi 37,493 waliofanya mitihani.

“Matokeo haya yanafanya Mkoa wa Arusha uwe umefaulisha kwa asilimia 70.6 na waliofaulu ni wavulana 12,608 na wasichana 13,856”alisema Itanisa.

Chanzo: Mwananchi, 28/12/2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO