Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA UWANJANI : NAMNA TAIFA STARS ILIVYOIFUINGA CHIPOLOPOLO 1-0 UWANJA WA TAIFA JANA

Hivi ndivyo Usomekavyo Ubao wa Matokeo katika Uwanja huu wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa kipindi cha kwanza cha mchezo katika ta Taifa Stars na Mabingwa wa Afrika,Zambia wana Chipolopolo.kipindi cha kwanza. Mchezo huo ulimalizika huku Taifa Stars ikiibuka na ushindi wa bao moja lililotiwa kimiani na Mrisho Ngassa mnamo dakika 45 ya mchezo kipindi cha kwanza.

 Mshambuliaji wa Taifa Stars,Hamis Mcha (katikati) akiwachachafya mabeki wa timu ya Zambia katika mchezo wa kirafiki unaoendelea hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa stars imeshinda goli 1-0.

Hamis Mcha (7) akiendelea kuwapa kazi mabeki wa timu ya Zambia.

 Mchezaji wa timu ya Zambia,Moses Phiri (9) akiingia kwenye lango la timu ya Taifa Stas,huku beki wa Stars,Aggrey Moris akijiandaa kukabiliana nae.

Mchezaji wa timu ya Zambia,Moses Phiri (9) akijaribu kutaka kumtoka beki wa Taifa stars,Salum Aboubakar wakati wa Mchezo wa Kirafiki kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar jana .Taifa stars ilishinda kwa bao moja lililotiwa kimiani na Mshambuliaji machachari,Mrisho Ngassa mnamo dakika ya 45 ya mchezo. 

Mchezaji wa timu ya taifa ya Zambia Chipolopolo James Chamanga akiruka juu kuwania mpira huku mchezaji wa timu ya Tanzania Taifa Stars Mrisho Ngasa akiuvizia, katika mchezo wa FIFA wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Timu ya Tanzania Taifa Stars iliifunga Chipolopolo ya Zambia goli 1-0 na kutoka kifua mbelea uwanjani , mfungaji wa goli hilo akiwa Mrisho Ngasa katika dakika ya 45 ya mchezo huo.

Mchezaji wa Taifa Stars Mrisho Ngasa akishangilia na kupongezwa na wenzake mara baada ya kufunga goli la mkwanza katika mchezo huo.

Wachezaji wa Taifa Stars wakitoka nje ya uwanja kwa mapumziko baada ya kipindi cha kwanza kuisha kwenye uwanja wa Taifa.

Mashabiki wa timu ya Taifa Stars wakishagilia mara baada ya Mrisho Ngasa kufungo goli la kwanza dhidi ya Chipolopolo katika mchezo huo

Kikosi cha timu ya Zambia kikiwa katika picha ya pamoja.

Mnazi Mkubwa wa Timu ya Yanga na Taifa Stars Heavy D. akinyanyua skafu yake yenye bendera na maneno ya Tanzania wakati wimbo wa taifa ukiimbwa kabla ya mchezo huo.

Kulia ni Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu nchini Zambia Kalusha Bwalya na mabalozi wa Zambia nchini Judith Kangoma-Kapijimpanga na Balozi Tanzania nchini Zambia Bi. Grace Mujumi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mchezo huo.

Mashabiki wa timu ya taifa ya Zambia wakishangilia timu yao katika mchezo huo.

Picha: MICHUZI BLOG

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO