Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Vita ya Sugu dhidi ya Rushwa kwa Madaktari Wa Rufaa Mbeya Yaanza Kuzaa Matunda, Daktari Apandishwa Kizimbani kwa Rushwa

DAKTARI wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa Mbeya,Paul Kisabi (32), anayetuhumiwa kwa kupokea rushwa ya sh 100,000

Hapa daktari huyo akiwa na maafisa wa takukuru wakiingia mahakamani

Hapa Dr huyo akiongea na wakili wake


Na: Mbeya Blog

DAKTARI wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa Mbeya,Paul Kisabi (32), amefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Mbeya, akikabiliwa na mashitaka mawili ya kushawishi na kupokea rushwa ya shilingi 100,000 kutoka kwa mgonjwa aliyefikishwa Hospitalini hapo baada ya kupata ajali.
Hatua hiyo imekuja baada ya Taasisi ya kuzui na Kuipambana na rushwa nchini takukuru, kumtia mbaroni daktari huyo juzi kwa tuhuma za kupokea rushwa ya kiasi hicho cha fedha baada ya kumuwekea mtego. Daktari huyo Kisabi amepandishwa kizimbani  majira ya saa 3:45 na kusomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Mbeya, Fransis Kishenyi, aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo ambayo imeibua hisia kali kwa wananchi.

Katika kesi hiyo namba 237 ya mwaka 2012, upande wa mashitaka uliongozwa na waendesha mashita wawili wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU), Joseph Mulebya na Nimrod Mafwele. Waendesha mashitaka hao walidai kuwa Disemba 19 majira ya asubuhi akiwa katika sehemu yake ya kazi katika kitengo cha upasuaji, mshitakiwa alitenda kosa la kwanza la kushawishi rushwa ya shilingi 200,000 kutoka kwa mgonjwa Meshack Brown, aliyefika hapo kwa lengo la kupatiwa matibabu.

Walisema katika kosa la pili, siku hiyo majira ya saa nane mchana akiwa katika baa moja iliyojulikana kwa jina la Victoria iliyopo Jijini hapa, mshitakiwa alitenda kosa lingine la kupokea hongo ya shilingi 100,000, huku akijua kuwa vitendo vyote hivyo ni kinyume na sheria. Walisema kuwa kwa mujibu wa sheria za taasisi hiyo, makosa yote yaliyotendwa na mshitakiwa yanaangukia kwenye kifungu cha 15 ibara ya 1 (a) cha sheria ya kuzuia rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Kabla kupangwa tarehe ya kutajwa tena kesi hiyo, Wakili wa mshtakiwa huyo, Ladislaus Rwekaza,aliiomba mahakama impe dhamana mteja wake akidai kuwa makosa yanayomkabili yanadhaminika. Hakimu Kishenyi alikubaliana na maombi ya Wakili Rwekaza kuwa mashtaka yote yanayomkabili mshtakiwa yanadhaminika na kusema dhamana yake iko wazi. Alimtaka mshtakiwa huyo kutimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini mali yenye thamani ya Sh,500,000, na kwamba awe na utambulisho wa barua kutoka kwa kiongozi wa serikali ya mtaa .

Hata hivyo mahakama ililazimika kuahirishwa kwa muda wa dakika 20 ili kutoa nafasi kwa mdhamini wa mshitakiwa kuleta barua hiyo baada ya kudai kuwa alikuwa ameisahau kwenye gari lililokuwa nje ya jingo la mahakama. Baada ya kupokea ombi hilo hakimu Kishenyi aliwahoji waendesha mashitaka kama wameridhika na hoja, ambao kwa pamoja walikubali kwa maelezo kuwa dhamana ni haki ya kisheria kwa mshitakiwa hivyo hawakuwa na pingamizi.

Mshitakiwa aliweza kutimiza masharti ya dhamana hiyo na hivyo kuachiwa huru hadi januari 7 mwaka 20013 ambapo kesi hiyo itaendelea kusikilizwa katika mahakama hiyo. Kwa mujibu wa kumbukumbu za mahama hiyo, mshitakiwa huyo Daktari Kisabi ni mmoja wa mashahidi wa kesi nyingine inayoendelea mahakamani hapo ya mtoto Anethi anayedaiwa kuchomwa moto katika mkono wake, kufungiwa ndani na kulazimishwa kula kinyesi chake na Shangazi yake.

Habari na Moses wa Mbeya Yetu Blog

ITAKUMBUKWA KWAMBA WIKI HII MBUNGE WA MBEYA MJINI, MH JOSEPH MBILINYI (CHADEMA) ALITANGAZA VITA YA WAZI NA MADAKATARI WOTE WANAOOMBA RUSHWA ILI KUTOA HUDUMA KATIKA HOSPITALI HIYO YA RUFAA.. MOJA YA TAMKO LAE LILIELEZA HIVI “NIMETANGAZA VITA NA MADAKTARI: KAZI IMESHAANZA HOSPITALI YA RUFAA-MBEYA NA TUTAKOMAA MWANZO MWISHO...KAMA MBUNGE NITAENDELEA KUTETEA HAKI NA MASLAHI YA MADAKTARI WENYE MAADILI KWA NGUVU ZANGU ZOTE...LAKINI NITAKUWA VITANI NA MADAKTARI WOTE WANAOCHAFUA TAALUMA YA UDAKTARI...”

BLOG HII INATOA PONGEZI ZA DHATI KWA HATUA HII NZURI YA KIONGOZI HUYU WA WANANCHI KUSAIDIA MAPAMBANO YA RUSHWA , TATIZO AMBLO LIMEKUWA KERO KUBWA KWA WANANCHI HASA WA HALI YA CHINI.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO