Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Waiba goli uwanja wa Sheikh Amri Abeid

KATIKA hali isiyo kawaida, watu wasiojulikana usiku wa Jumapili wiki iliyopita, wameiba mabomba ya kuunganishia magoli ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Wizi huo umewaacha wadau wengi wa soka jijini hapa wakiwa na maswali mengi ya kujiuliza kuliko majibu, hasa ukizingatia kwenye uwanja huo kuna walinzi.Tukio hilo linalodaiwa kufichwa kinamna, limewahusisha baadhi ya walinzi wa uwanja huo waliokuwa zamu siku hiyo.

Wezi hao kwa kujiamini, wanadaiwa kuingia ndani ya uwanja huo na kukata mabomba ya kuunganishia magoli hayo na kutokomea nayo.Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa, hii siyo mara ya kwanza wezi kuingia ndani na kuiba mali za uwanja huo.

Inadaiwa kuwa, tangu kuondoka Meneja wa Uwanja huo, Mashaka Ngwabi kumeufanya kupoteza hadhi yake ikiwa ni pamoja watu kuingia ovyo uwanjani.“Tangu ameondoka Ngwabi, uwanja umeporomoka hadhi yake,” alisema mdau mmoja wa soka ambaye hakutaja jina lake kuandikwa kwenye gazeti.

Mwananchi ilishuhudia walinzi wa uwanja huo wakihaha kuwasaka wezi na mabomba hayo na walipoulizwa walionyesha kushtushwa.Baadhi ya walinzi walisema wizi huo umechangiwa kwa kiasi kikubwa na wenzao ambao siyo waaminifu.

Alipotafutwa Katibu wa CCM Arusha, Mary Chatanda kutoa ufafanuzi juu ya tukio hilo hakupatikana na alipotafutwa meneja wa uwanja huo aliyejulikana kwa jina moja la Bokasa, aligoma kuzungumzia wizi huo.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO