Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Lema aipaisha CHADEMA

SAM_5021

USHINDI wa Rufaa aliyofungua Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), kupinga kuvuliwa ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, umekipaisha chama hicho na kukiongezea umaarufu maradufu.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili hasa katika Mkoa wa Arusha ambako CHADEMA ina wafuasi wengi, umebaini kuwa nguvu ya chama hicho imezidi kuimarika.

Wadadisi wa mambo ya siasa waliozungumza na gazeti hili, walibainisha kuwa tangu Lema awe nje ya ubunge na kupunguza kasi yake ya kukijenga chama mkoani hapo, umaarufu wa chama hicho ulishuka kiasi cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanza kutamba kwamba watairejesha Arusha mikononi mwao.

“Ndiyo maana hata Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake walipowasili Arusha, walipata watu wengi tofauti na mikutano yao ya awali ambapo haikuwa rais kwa CCM kupata watu wengi kiasi hicho. Ujio wa Lema kwenye ubunge wake hakika umekipaisha zaidi chama hicho,” alisema mmoja wa makada wa CCM ambaye hakupenda jina lake litajwe.

Hata hivyo, hatua ya Lema kurejeshewa ubunge, haikuipaisha CHADEMA mkoani Arusha tu, bali pia hata katika mikoa mingine.

Sababu kubwa inayotajwa na duru za siasa za kuongezeka umaarufu wa CHADEMA, ni hukumu ya awali ambayo imeonekana dhahiri kwamba ni ya uonevu na ilikuwa na msukumo wa vigogo wa serikali.

“Ukiangalia hoja zilizotumika na Mahakama ya Rufaa, unaweza kuhoji kama kweli Jaji Gabriel wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha alitumia sheria na vigezo gani kumvua ubunge Lema. Hii ndiyo imewafanya watu wengi kuionea huruma CHADEMA na kufanya ionekane inaonewa,” alisema mchambuzi mwingine wa masuala ya siasa.

Mbali ya rufaa hiyo kuipaisha CHADEMA, pia imevunja nguvu ya kundi la mashushu wa ndani na nje ya chama hicho, ambao katika siku za hivi karibuni walishika kasi ya kuendesha kampeni na harakati chafu za kutaka kuisambaratisha CHADEMA.

Mfano wa kundi hilo ni lile la waasi kutoka ndani ya Umoja wa Vijana wa CHADEMA (BAVICHA), ambao wamekuwa wakiendesha kampeni chafu dhidi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa kwa hoja dhaifu kuwa ni mamluki kwa vile anaendelea kumiliki kadi ya CCM.

“Leo hata wale vijana waliokuwa wakisambaza sumu kwamba Dk. Slaa ana kadi ya CCM, hawana nguvu tena kwani wanaonekana ni watu wale wale wanaoionea CHADEMA bila sababu za msingi,” alisema mchambuzi huyo wa masuala ya kisiasa.

Katika siku za hivi karibuni, kundi la mashushu kwa kuwatumia baadhi ya wanachama wa CHADEMA, kusambaza sumu kwa lengo la kuisambaratisha.

Mashushu hao wamekuwa wakiwafuata baadhi ya makada maarufu wa CHADEMA na kuwapa fedha za kuzunguka mitaani kukivuruga.

Na Tanzania Daima

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO